Home LOCAL TAASISI ZA DINI ZATAKIWA KUANZIASHA PROGRAMU ZA HUDUMA YA KIJAMII

TAASISI ZA DINI ZATAKIWA KUANZIASHA PROGRAMU ZA HUDUMA YA KIJAMII

Na:  WMJJWM, DAR ES SALAAM

Taasisi za Dini zimetakiwa kuimarisha huduma za kimwili na kiroho kwa waumini wao kwa kuanzisha na kuboresha programu zenye shughuli za maendeleo ya kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Gwajima wakati akizungumza na waamini wa kanisa la THE WELL OF SANCTUARY kwenye ibada ya kuwekwa wakfu Askofu wa kanisa hilo Benedict Felix Lyimo pamoja na watumishi wengine wa kanisa hilo mkoani Dar es salaam Julai 30, 2023.

Dkt. Gwajima ameeleza, ni wajibu wa kanisa na madhehebu mengine ya dini kushirikiana na Serikali katika kukemea mmomonyoko wa maadili na kupiga vita vitendo vya rushwa ya kila aina.

“Kupitia mafunzo mbalimbali yanayolenga uchumi, ujasiriamali, uchumba na ndoa na hata maisha kwa ujumla haya ni mambo muhimu kwa wanawake hususani vijana wanaohitaji sana ujuzi na mwongozo wa kanisa” amesema Dkt. Gwajima.

Aidha, Waziri Dkt. Gwajima amepongeza juhudi za kanisa la THE WELL OF SANCTUARY kwa malezi bora ya watoto kupitia kituo cha kulea watoto mchana.

Awali akizungumza na waamini waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Danstan Maboya ambaye ameongoza zoezi la kuwekwa Wakfu Viongozi wa Kanisa hilo, ameitaka jamii kuheshimu majukumu ya watumishi wa Mungu kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here