Home BUSINESS SUA YADAHILI WANAFUNZI ZAIDI YA 6000 MAONESHO YA TCU JIJINI DAR

SUA YADAHILI WANAFUNZI ZAIDI YA 6000 MAONESHO YA TCU JIJINI DAR

Mkuu Kitengo Cha elimu ya Kujiendeleza, kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)Dkt.Emmanuel Malisa, amesema kuwa Chuo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kudahili wanafunzi zaidi ya 6000, wakati wa Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyofungwa rasmi Julai 22, 2023 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi Julai 18, mwaka huu yalitoa fursa kwa wananchi mbalimbali hususani vijana kutembelea katika Banda lao, na kupata maelezo ya kina juu ya kozi zinazotolewa chuoni hapo na kwamba, kumekuwa na mwitiko mkubwa kwa wananchi hao, na kuweza kufanya Udahili wa Papo kwa hapo.

“Kutokana na mafunzo ya vitendo, yametupelekea watu wanaotembelea Banda letu, kufanya kudahili moja kwa moja hapa, hii inatokana na elimu nzuri tunayotoa katika chuo chetu, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya shahada za awali, mafunzo ya uzamili, na shahada za juu.

“Vile vile tunafanya tafiti mbalimbali na kutoa ushauri wa kitaalam kwa wahitaji. Hapa tupo tunaonyesha matokeo ya tafiti zetu ambazo tunazifanya pale SUA, lakini pia kitu kikubwa ambacho tunajivunia ni mafunzo ya vitendo kwamba vijana wanapokuja chuoni kwetu wanafanya vitendo kweli kweli, kwa hiyo ukipita kwenye Banda letu utakachokiona ni zao la kile wanachofundiashwa na kufanywa na vijana wetu,” amesema Dkt.Malisa.

Aidha ameishukuru Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) kwa kuwapa heshima ya Cheti cha ushiriki katika maonesho hayo, na kwamba ni chachu kwa ajili ya wao kufanya vizuri zaidi.

Kwa upande wake Afisa Mawasiliano na Masoko SUA, Bi. Suzana Magobeko amesema kuwa Chuo hicho kina ubora  wa juu kitaaluma, na kwamba ni Kikongwe nchini Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo amewasihi wadau na wananchi wote kufika katika Chuo hicho kupata Elimu ya masuala ya Kilimo na Mifugo.

Pia amesema kuwa kwa wale wahitimu ambao hawakuweza kufika katika Maonesho hayo, wanaweza kupata taarifa zaidi kwa kutembelea tovuti ya Chuo www. sua.ac.tz na wale wanaotaka kujisajili wanaweza kuingia kwenye link maalum ambayo ni http://197.250.34.38:8389/index.php/registration

Previous articleKENYA YAIPONGEZA STAMICO, YAAHIDI KUENDELEA KUJIFUNZA KWAKE
Next articleMUSONDA AIPA YANGA FURAHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here