Home LOCAL PROF. MKENDA AIPONGEZA UDOM KWA UMAHIRI WA PROGRAMU ZAKE

PROF. MKENDA AIPONGEZA UDOM KWA UMAHIRI WA PROGRAMU ZAKE

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Bi. Rose Joseph (kushoto), mara baada ya waziri huyo kufika katika Banda la Chuo hicho kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya katika Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Chuo Kikuu cha Dodoma, kimeweka kambi katika maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea kwenye Banda lao, na kufanya Udahili wa papo kwa hapo, ambapo zaidi ya Programu 80 zinatolewa katika ngazi ya Shahada za Awali na  Programu zaidi ya 56 kwa ngazi ya Shahada za Umahili (Postgraduate Diploma, Masters & PhD) 

Fani zinazotolewa UDOM, ni pamoja na Udaktari, Uchumi, Sheria, Sosholojia, Utawala wa Biashara, Biashara na Uhasibu, Biashara katika Utawala na Rasilimali Watu, ujasiriamali, Biashara ya Kimataifa, Utalii, Masoko, Mazingira, Takwimu, Ununuzi na Ugavi, Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA), Jiolojia, Kemia, Madini, Petroli, Nishati Mbadala, Elimu, lugha, Uhusiano wa Kimataifa, ikolojia, Uandishi wa Habari na Mahusiano ya Umma, fizikia, na nyinginezo.

Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo, “Kukuza ujuzi nchini kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwa uchumi imara na shindani” yameshirikisha Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu zaidi ya 80 ambapo, yanatarajiwa kuhitimishwa rasmi Julai 22, Mwaka huu.

Previous articleTANZANIA YABAINISHA HATUA INAZOCHUKUA KUELEKEA USAWA WA KIJINSIA
Next articleUJUZI NA UMAHILI UNAOTOLEWA NA CHUO CHA BAHARI, KUWAKWAMUA VIJANA NA UKOSEFU WA AJIRA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here