Home BUSINESS MKAA WA STAMICO WAINGIA KWENYE MKAKATI WA TAIFA WA NISHATI SAFI YA...

MKAA WA STAMICO WAINGIA KWENYE MKAKATI WA TAIFA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Mhandisi Mtaalam wa Uchenjuaji Madini wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Happy Mbenyange, kizungumza na mwananchi aliyefika katika Banda la Taasisi hiyo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo kwenye Maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR S SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Shririka la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse amesema kuwa Bidhaa yao ya mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) tayari imeingia kwenye mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia, na kwamba ifikapo mwaka 2033 kila mtu anatakiwa aachane na matumizi ya mkaa wa miti na  kuni.

Dkt. Mwasse amebainisha hayo hivi karibuni alipozungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia, na kwamba ifikapo mwaka wa 2024 Taasisi zote zinatakiwa ziachane na matumizi ya mkaa wa miti pamoja na kuni.

“Tumefanya utafiti kwa miaka mitatu kwa kuzihusisha taasisi zetu za utafiti ikiwemo COSTECH, Vyuo Vikuu, na TIRDO. Sambamba na hilo, pia tumefanya uzalishaji pale TIRDO ambao ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa, hatukuishia hapo tukawaalika na wenzetu wa Viwango TBS, ambao walienda kuuchunguza na mwisho wa siku tumepata cheti cha TBS kwamba Bidhaa hii sasa imekidhi viwango kwa matumizi ya Binadamu” amesema Dkt. Mwasse.

Ameongeza kuwa katika Maonesho ya Sabasaba mwaka huu STAMICO imeendelea kutoa elimu kwa wanachi juu ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo mkaa huo, na kamba hivi karibuni Bidhaa hiyo itaanza kupatika katika mikoa mbalimbali Bara na Visiwani. 

“Tupo kwenye maonesho hayo kwaajili ya kuonesha Biashara zetu na shuguli tunazozifanya, kama mnavyoona tumekuja hapa kuwaonesha watanzania bidhaa tulizo nazo ikiwemo mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) na tumelitolea wasilisho maalum ili kila mmoja awe na uelewa”

“Wito wangu, watanzania waelewe kwamba sasa hivi tunakwenda kwenye Dira mpya na sera ya nishati safi za kupikia ambayo inaelekeza kuachana na matuimizi ya mkaa wa miti au kuni, na kuhakikisha kwamba tunatunza mazingira yeu. Tujiepushe na ukataji miti, hii itapelekea kuachana kabisa na changamoto za Mabadiliko ya tabia nchi” Ameongeza.

STAMICO ni Shirika la Serikali chini ya Wizara ya Madini ambalo lilianzishwa kwa sheria ya Mashirika ya Umma sura 257 kupitia agizo la Uanzishwaji wa Shirika la Madini la Taifa namba 163, mwaka 1972 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2014.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JULAI 10, 2023
Next articleSHAWEJI AWATAKA UWT KINONDONI KUANZA MAPEA MAANDALIZI YA UCHAGUZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here