Home LOCAL MAONESHO YA TCU KUFUNGULIWA RASMI LEO JIJINI DAR

MAONESHO YA TCU KUFUNGULIWA RASMI LEO JIJINI DAR

Mkurugenzi wa Udahili na Menejimenti ya Data, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Dkt. Kokuberwa Katunzi Mollel, akizumza na waandishi wa habari (hawamo pichani), katika viwanja vya mnazi mmoja kuhusu Maoesho ya Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, yanayoratibiwa na (TCU), yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi leo Julai 18, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanatarajiwa kufunguliwa rasmi leo Julai 18, 2023 katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8 mchana.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari jana Julai 17, 2023 viwanjani hapo, Mkurugenzi wa Udahili na Menejimenti ya Data, Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU), Dkt. Kokuberwa Katunzi Mollel, amesema Maonesho hayo yamevikutanisha pamoja Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu takribani 86 kwa lengo la kutoa fursa kwa wanachi hususani wanafunzi kuchagua vyuo wanavyovyitaka, na kufanya Udahili wa papo kwa hapo.

Aidha ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yameshirikisha Taasisi nyingine zilizoshiriki kutoa huduma na elimu mbalimbali kwa wananchia ambazo ni,  Bodi ya Mikopo, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Baraza la wataalamu la Manesi na Wakunga, na Baraza la Wanasheria, ambaao wameshiriki  kutoa huduma na kutangaza kazi wanazozifanya.

“Pia tupo na Mawakala ambao wanasaidia watanzania kupata nafasi za masomo nje ya nchi, kwa hiyo nao wanashiriki katika maonesho haya na wanatoa huduma zao hapa.

“Umuhimu wa maonesho haya ni kwamba, kipindi hiki kama mnavyofahamu matokeo ya kidato cha sita yametoka, kwa hiyo ni fursa muhimu kwa waombaji waliomaliza kidato cha sita kuja hapa uwanjani, kwanza kuvifahamu vyuo ambavyo vitadahili mwaka huu, lakini pia kuja kufahamu fursa mbalimbali.

“Kikubwa hizi Taasisi zilipo hapa zinaweza kuwasaidia Kutuma maombi moja kwa moja kupitia mifumo yao ya kielectroniki, kwa sababu maombi ya kujiunga na vyuo yanatumwa kwa njia ya mtandao, na wakifika hapa ni rahisi kukutana na vyuo husika wakawaelekeza namna ya Kutuma maombi, lakini watawaelimisha zaidi sifa stahiki na programu zilizopo vyuoni” ameeleza Dkt. Mollel.

Ameongeza kuwa kwa wale waliomaliza Vyuo, TCU wapo hapo kutoa huduma ambapo, moja ya huduma wanazotoa ni pamoja na kutambua vyeti vyao, au tuzo walizonazo kwa wale waliosoma nje ya nchi.

“Kwa hiyo wakifika kwenye Banda letu tutawapa maelekezo ya kina kuhakikisha kwamba tuzo zao walizozipata nje ya nchi zinatambuliwa, vilevile kwa wale wanaokwependa kusoma nje ya nchi, tunawasihi wafike Banda la TCU, ili wapate maelezo jinsi ya kupata hati, ili kutokakuwa na pingamizi, kwa sababu kwanza inampa mzazi au mwanafunzi uhakika wa chuo anachokwenda kusoma kama kinatambuliwa na wenzetu katika nchi yao.

“Lakini pia programu atakazokwenda kusoma zina tambuliwa, na kama yeye ana sifa za kusoma programu hiyo, inaweza kumrahisishia sana, kuliko kwenda kwenye sehemu ambayo haina uhakika kwani atakuwa amepoteza muda na fedha,” ameongeza Dkt. Mollel.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JULAI 18-2023
Next articleRAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA HUNGARY MH. KATALAN NOVAK IKULU DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here