Home LOCAL MAJALIWA ATOA SIKU 7 WATENDAJI TARURA, DAWASA KUKAMILISHA BARABARA MUHIMBILI.

MAJALIWA ATOA SIKU 7 WATENDAJI TARURA, DAWASA KUKAMILISHA BARABARA MUHIMBILI.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa siku saba Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Mikinga na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiza (DAWASA) Lydia Ndibalema wawe wamekamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.

Barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu linalotoka katika hospitali hiyo ilipaswa kuwa imekamilika mwishoni wa mwezi wa sita 2023.

Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana ili kuepusha adha kwa wagonjwa na wanafamilia wanaoitumia barabara hiyo kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Julai 24, 2023 alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara hiyo.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 24-2023
Next articleSIMBA SC YAMUUZA SAKHO UFARANSA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here