Home LOCAL KISWAHILI KIMEVUKA MIPAKA, REDIO NA RUNINGA 38 DUNIANI ZINARUSHA MATANMGAZO KWA LUGHA...

KISWAHILI KIMEVUKA MIPAKA, REDIO NA RUNINGA 38 DUNIANI ZINARUSHA MATANMGAZO KWA LUGHA YA KISWAHILI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwahutubia  wataalamu wa lugha ya kiswahili katika Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF  na vyombo mbalimbali  vya habari uluofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kilele Cha siku ya Kiswahili Duniani

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akikagua maonesho ya waswahili Katika mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na wataalamu wa lugha ya kiswahili na waandishi wa  vyombo vya habari mbalimbali uliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kilele Cha Siku ya Kiswahili Duniani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Said Yakub akizungumza Katika mkutano wa Wataalam wa lugha ya kiswahili na wahariri Kutoka  Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF uliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kilele Cha Siku ya Kiswahili.

     

Na: Eleuteri Mangi, WUSM, Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amewataka Wahariri kushirikiana na mabaraza ya Kiswahili ya BAKITA na BAKIZA ili kuendeleza lugha ya Kiswahili.

Amesema kuwa lugha ya Kiswahili imevuka mipaka na sasa kuna redio na runinga 38 duniani zinazorusha matangazo yao kwa kutumia lugha ya Kiswahili ndiyo maana kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani inahimiza kuwa “Kiswahili Chetu; Umoja Wetu”.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema lugha ya Kiswahili ipewe hadhi na ukubwa wake na mahali bora zaidi kuanzia ni Jukwaa la wahariri ambao wanafanyakazi ya kutoa mwelekeo wa lugha na mambo mbalimbali kwa kusoma, kutazama na kusikiliza.

Naibu Waziri Mwinjuma amesema hayo Julai 4, 2023 Mjini Zanzibar wakati wa mkutano na Jukwaa la Wahariri kuelekea Siku ya Kiswahili Duniani mada ikiwa ni “Nafasi ya Wahariri Wakuu katika kusimamia matumizi ya Kiswahili sanifu katika vyombo vya Habari”.

“Hamu yangu ni kukaa kwenye mkutano huu kuanzia mwanzo hadi mwisho bila kusikia neno la lugha nyingine zaidi ya lugha sanifu na sahihi ya Kiswahili” amesema Naibu Waziri Mwinjuma.

Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili yam waka 2023 ni ya pili bbada ya kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2022 ambayo ni siku maalum ya kuadhimishwa lugha hiyo baada ya kutangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021.

Previous articleHEMED: WANAHABARI KUCHANGAMKIENI FURSA ZITOKANAZO NA KISWAHILI
Next articleCHUO KIKUU MZUMBE WATOA SHUKRANI KWA WADAU WANAOENDELEA KUCHANGIA UJENZI WA BWENI LA WANAFUNZI WA KIKE NDAKI YA MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here