MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amewasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza ziara katika mikoa ya Manyara, Mara, Simiyu na Tabora ambako akiwa katika mikoa hiyo atakagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho pamoja na kuzungumza na wananchi.
Pia atashiriki vikao vya ndani ya Chama kwa kuzungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali sambamba na mikutano ya hadhara yenye lengo la kuelezea masuala mbalimbali yanayohusu kutekelezwa kwa Ilani ya Uchaguzi Mkuu.
Katika ratiba ya ziara ya Kinana Julai 23 ,2023 baada ya kuwasili Dodoma atakwenda wilayani Kondoa ambako atashiriki mkutano mkuu wa jimbo la Kondoa.
Aidha Julai 24, 2023 Makamu Mwenyekiti Kinana atawasili wilayani Babati mkoani Manyara ambako atashiriki mkutano wa Kamati ya siasa ya Mkoa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Simanjiro.
Julai 25, 2023 atakwenda mkoani Mara na Julai 26 ,2023 atashiriki vikao vya Chama , kukagua ukumbi wa CCM na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi huo na kisha atafanya mkutano mkubwa wa hadhara.
 Wakati Julai 27,2023 Kinana atapokelewa Bariadi mkoani simiyu tayari kwa kushiriki mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ,pia atakuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM Mkoa.Baada ya hapo atapata nafasi ya kuzungumza na waganga wa tiba asili na kisha atashiriki mkutano wa hadhara.
Kinana atahitimisha ziara yake mkoani Tabora ambapo atapokelewa Julai 29, 2023 na Julai 30,2023 atashiriki mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa na baadae mkutano wa hadhara .
Ziara hiyo ya Kinana itahitimishwa Agosti 1,2023 na kurejea jijini Dar es Salaam kuendeelea na shughuli nyingine za kichama.