Home LOCAL KINANA AWATULIZA WANANCHI UFUMBUZI BEI YA PAMBA, TEMBO KUVAMIA MAKAZI YA WATU.

KINANA AWATULIZA WANANCHI UFUMBUZI BEI YA PAMBA, TEMBO KUVAMIA MAKAZI YA WATU.

 

Na: Mwandishi Wetu, Itilima

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amewaeleza wananchi wa Itilima jinsi serikali itakavyotatua changamoto ya bei ndogo ya pamba nchini na uvamizi wa tembo katika makazi ya wananchi.

Kinana ametoa kauli hiyo jana Julai 28, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Laini A wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu akiwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, uhai wa Chama na kusikiliza changamoto za wananchi.

Akiwa mkoani humo Kinana alipokea malalamiko ya wananchi hasusan wakulima wa pamba kwamba wanatumia gharama kubwa kulima zao hilo, lakini changamoto inayowakabili ni bei ndogo, hivyo walimuomba awasaidie kufikisha kilio chao kwa Chama na serikali upatikane ufumbuzi wa bei ya pamba.

Kinana baada ya kuwasikiliza wakulima hao aliowapa nafasi ya kuuliza maswali, alisisitiza kwamba kuondoa changamoto ya bei ndogo ya pamba, serikali kuu ijitahidi kutengeneza viwanda vya kutengeneza nyuzi, kuchakata pambana na kutengeneza nguo kusiwe na ulazima wa kupeleka pamba nje ya nchi.

Kuhusu malalamiko ya wananchi kuvamiwa na tembo ambao wamekuwa wakisababisha wananchi kupoteza maisha, Kinana alisema amekaa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa wilaya, mkoa na maofisa wa uhifadhi wanyamapori kuzungumzia tatizo la wananchi kuvamiwa na kuuliwa na tembo.

“Tumezungumza kuhusu fidia kwa watu wanaokufa, tumezungumzia mipaka kati ya wananchi na hifadhi, nitakaporudi nitazungumza na Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa Ardhi hili jambo hili lifanyiwe kazi.” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here