Home LOCAL KINANA AHIMIZA UMOJA, MSHIKAMANO KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

KINANA AHIMIZA UMOJA, MSHIKAMANO KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, amewashauri viongozi wa Chama hicho katika ngazi zote kuendeleza umoja ili kwenda katika Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 wakiwa wamoja na kuibuka washindi pamoja.

Kinana ameyasema hayo leo Julai 23, 2023 wakati akizungumza na viongozi wa CCM katika kikao cha ndani cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa mkoabi Dodoma.

“Napongeza kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa CCM hususan katika ngazi kitongoji, Kijiji, mtaa na Kata kwa kazi nzuri mnayoifanya. Mwakani ni mwaka wa Uchaguzi, hivyo naamini wana CCM tutakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mtaa mwaka 2024 tukiwa kitu kimoja, tukifanya kampeni wamoja na tutaibuka na ushindi tukiwa wamoja, hivyo hivyo katika uchaguzi mkuu mwaka 2025,” amesema Kinana.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba Chama pia kinatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotelewa na viongozi wa CCM katika ngazi za kata, vitongoji, vijiji, wilaya na mkoa kwani wao ndio wanaokutana na wananchi na wakati wa uchaguzi ndio wanaokwenda kuomba kura.

Pia, amewapongeza madiwani wanaotokana na CCM ambao wamekuwa wakisimamia ngazi ya Kata na wamekuwa wakifanya hivyo bila ya kuwa na mshahara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here