Home LOCAL KINANA AFURAHISHWA MIKAKATI YA KUWAINUA, KILIMO WAKULIMA

KINANA AFURAHISHWA MIKAKATI YA KUWAINUA, KILIMO WAKULIMA

 

Tabora

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo na mchango wake katika maendeleo ya nchi, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kuboreshwa.

Akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Tabora, Kinana amezungumzia sekta ya kilimo hususan hatua zinazochukuliwa na serikali kutatua changamoto za wakulima.

“Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeeleza yanayoendelea kwenye kilimo, amezungumzia mambo mbalimbali ya kilimo, kama hujamsikia na ukasikiliza kero peke yake unapata hisia kuna kero hazishughulikiwi, lakini ukisiliza kwa makini unaona kuna kazi inafanyika, kuna ufumbuzi unaotolewa kwa matatizo hayo.

Yako mambo hayawezi kufanikiwa mara moja, ninyi ni mashahidi Wizara ya Kilimo ni muhimu kwa Watanzania kwani asilimia kubwa wanaishi vijijini, maisha yao yanategemea kilimo. Rais Samia Suluhu Hassan wakati anachukua nchi hii Wizara ya Kilimo ilikuwa ikipata Sh.bilioni 260, lakini na leo inapata Sh. trilioni moja.

Alifafanua kuwa, miradi mingi ama ilisimama au ilipuuzwa, lakini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa mara ya kwanza maofisa ugani wameajiriwa, vitendea kazi vipo vya kutosha, pembejeo zinatolewa kwa ruzuku kutoka serikalini kwa mazao yote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here