Home BUSINESS DP WORLD HAITAMILIKISHWA ARDHI YA TANZANIA.

DP WORLD HAITAMILIKISHWA ARDHI YA TANZANIA.

Kiongozi wa majadiliano ya serikali katika suala la majadiliano ya Mkataba wa Bandari, Hamza Johari ametoa ufafanuzi wa vipengele mbalimbali, akisema mwekezaji DP World hatomilikishwa ardhi ya Tanzania na badala yake atakodishwa.

Johari ambaye ni Mtaalamu mbobevu wa mikataba ya Kimataifa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga, ametoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam katika mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania, uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt, Klimanjaro.

Katika ufafanuzi huo amesema, hivi sasa bado mkataba wa bandari haujasainiwa na kilichopo sasa ni makubaliano ambayo yanajenga msingi wa mkataba ambao utaandaliwa kwa ajili ya kuongoza ushirikiano wa kiuchumi kati ya serikali ya Tanzania na Dubai.

Amesema iwapo mkataba huo ukianza utekelezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam, italeta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa manufaa ya watanzania kupitia mwekezaji DP World.

Aidha, amesema nchi haijauzwa na kwamba mwekezaji DP world atakuwa na asilimia 8 tu katika uendeshaji wa baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dar es salaam.

Na amesisitiza kuwa DP world bado hajaanza kufanya kazi nchini Tanzania kama inavyodaiwa na wapotoshaji kuhusu suala la uwekezaji huo.

Aidha, Johari amesema suala la uwekezaji wa kampuni ya DP World halipo kwenye mambo ya Muungano wa nchi saba zinazounda Umoja wa Falme za Kiarabu, hivyo katiba yao imetoa haki kwa moja ya nchi wanachama kuingia kwenye ushirikiano na nchi yoyote.

Amesema majadiliano hayo tayari yameridhiwa na bunge ili kuyalinda, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.

Pamoja na mambo mengine, amesema majadiliano hayo yaliyoanza tangu mwaka 2018, yana kipengele kinachowezesha kama mkataba utasainiwa kutakuwa na nafasi ya marekebisho kwa pande zote mbili.

Aidha, amefafanua kuwa kuna kipengele katika majadiliano kinachoruhusu mwekezaji mwingine kuwekeza katika bandari ya Dar es salaam na serikali.

Akifungua kikao hicho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa, amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es salaam kupitia kampuni ya DP world utalinda ajira za wazawa na kupunguza meli kukaa Nangani.

Pia DP world hatohusika na Gati namba 8 hadi 11 na pia hatohusika na boya la mafuta pamoja na hatahusika na Bandari ya Tanga, Mtwara na Bagamoyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here