Home BUSINESS DKT. KIJAJI: JUMLA YA MIRADI 522 YA UWEKEZAJI IMESAJILIWA NCHINI

DKT. KIJAJI: JUMLA YA MIRADI 522 YA UWEKEZAJI IMESAJILIWA NCHINI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto), akimkabidhi nyaraka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, (kulia), aliyepewa dhamana ya kusimamia Masuala ya Uwekezaji nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 28, 2023 katika Ofisi za kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza na Waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa zoezi la makabidhiano ya Majukumu ya Uwekezaji, ambayo sasa yamehamishiwa katika wizara mpya Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 28, 2023 katika Ofisi za kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo akizungumzia mambo manne muhimu aliyokabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji katika hafla hiyo iliyofanyika leo Julai 28,2823 Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya rais mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida (aliyesimama) akizungumza alipokuwa akitoasalamu za utangulizi katika mkutano huo.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa jumla ya miradi 522 imesajiliwa katika sekta mbalimbali hapa nchini, kuanzia kipindi cha mwezi januari 2022 hadi hivi sasa.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo leo Julai 28,2023 katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya majukumu ya Uwekezaji kati yake na Waziri wa Wizara hiyo Prof. Kitila Mkumbo ambaye kipande cha Uwekezaji kimehamishiwa kwenye Wizara yake,

Halfa hiyo imefanyika katika Ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Kijaji alitoa taarifa fupi ya hali ya uwekezaji nchini, na kumkabidhi Prof. Mkumbo mambo manne ambayo ataendelea kuyatekeleza kuendelea  kuvutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini.

“Kwa mwaka uliopita tangu nimeaminiwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, na kupewa kipande hiki cha uwekezaji tumesajili miradi 522 kuanzia januari 2022 mpaka sasa ninapokukabidhi sekta hii ambayo ni muhimu kwa nchi.

“Usajili wa miradi hii itawezesha upatikanaji wa ajira 72,000 na kupunguza changamoto ya ajira nchini, lakini pia katika uwekezaji huu, nchi itapata mapato na kuinua uchumi wa Watanzani. Mamesema Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema kuwa kuundwa kwa Wizara hiyo kumetokana na dhamira njema aliyonayo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kukuza Sekta ya Uwekezaji na kufungua milango zaidi ya Wawekezaji wengi kuja nchini.

Aidha amebainisha kuwa yapo mambo mamnne ya kuyaendeleza ambayo mchakato wake ulishaanza ikiwemo Mchakato wa Mabadiliko ya Sera ya uwekezaji ya mwaka 1996.

“Kufuatia auamzi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, wa kuunda Wizara mpya ya Mipango na Uwekezaji, leo Waziri wa Viwanda na Biashara amenikabidhi kipande cha Uwekezaji ambacho kilikuwa chake na amenikabidhi mambo manne ikiwemo Mchakato wa Mabadiliko ya Sera ya uwekezaji ya mwaka 1996, amenikabidhi Sheria Mpya ya Uwekezaji na Kanuni zake ya mwaka 2022 ambayo ilipitishwa Bungeni hivi karibuni”, Prof. Kitila Mkumbo.

Amesema katika makabidhiano hayo pia amekabidhiwa Bajeti ya mwaka 2023/2023 kwenye kipande cha uwekezaji akibainisha kuwa jukumu la Wizara hiyo ni kuvutia wawekezaji ili kukuza uchumi wa nchi

Wizara hiyo ina jukumu kubwa la kuendelea kuvutia wawekezaji wakubwa kutoka sehemu mbalimbali Duniani na ndani ya nchi, huku akitaja Utulivu na Utashi wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya kisheria ni mambo ambayo yanavuta wawekezaji wengi kutoka nje ya nchi.

Previous articleWATOTO WALIOWEKA REKODI GGML KILICHALLENGE,WANG’ARA SIKU YA MASHUJAA
Next articleTAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA RIBA YA MIKOPO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here