Mkuu wa Ndaki ya Mbeya ,Chuo Kikuu Mzumbe amewashukuruu Wadau wote wanaoendelea kuchangia harambee ya ujenzi wa hosteli ya Wanafunzi wa kike katika Ndaki hiyo na kuwaomba Wadau wengine kuendelea kuunga mkono uchangiaji wa ujenzi huo ambao ulizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera Mei Mwaka huu.
Akizungumza wakati wa Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Prof. Henry Mollel amesema anaendelea kuwakaribisha Watanzania wote kutembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam maarufu kama Saba saba
Prof.Mollel amewahimiza Wanafunzi waliomaliza Chuo hicho miaka ya nyuma (Alumni) ambao wapo nchi nzima na walio nje ya nchi ,Wadau wa Elimu na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Chuo hicho kuunga mkono juhudi hizo na kuhakikisha watoto wa kike wanasoma kwenye mazingira mazuri.
Prof. Mollel amesema Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni mwa vyuo vinavyotoa Mafunzo mbalimbali ikiwemo masomo ya Biashara, Utawala, Sheria, Uhasibu, Sayansi na Teknolojia ambapo wanateknolojia mbalimbali ambazo wamekuwa wakizianzisha katika chuo hicho.
“Tukifanikiwa kujenga tutahamasisha na kuongeza udahili wa wanafunzi , naamini kwamba kila Mzazi atavutiwa kuona mtoto wake akipata elimu kwenye Chuo kizuri kama Mzumbe lakini mtoto wake wa kike atapata mazingira bora ya kuishi na kuendelea na masomo yake.” Amesema
Prof. Mollel amewaomba wahitimu wa Chuo Kikuu mzumbe, wadau wote wa elimu Tanzania kuunga mkono kwa kuchangia ujenzi huo kwa kiasi chochote atakachokuwa nacho kuchangia kupitia namba maalumu ya kuchangia control namba994180331310 ili kufanikisha ujenzi huo.