Home BUSINESS CHUO KIKUU MZUMBE CHAKARIBISHA WANAFUNZI KUJIUNGA NA CHUO HICHO KWA  KOZI MBALIMBALI

CHUO KIKUU MZUMBE CHAKARIBISHA WANAFUNZI KUJIUNGA NA CHUO HICHO KWA  KOZI MBALIMBALI

Na: Neema Adriano, Dar-es-Salaam

Chuo Kikuu cha Mzumbe ni miongoni mwa vyuo vinavyotoa Mafunzo mbalimbali ikiwemo masomo ya Biashara, Utawala, Sheria, Uhasibu, Sayansi na Teknolojia ambapo wanateknolojia mbalimbali kuwa na vijana wao ambao wamekuwa wakizianzisha katika chuo hicho

Akizungumza wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe anaeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri, Dk. Eliza Mwakasangula amesema anawakaribisha Watanzania wote waweze kutembelea banda lao lililopo katika Viwanja hivyo ambayo yanaendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

” Katika Chuo chetu tunatoa huduma mbalimbali, ikiwemo kudahili wanafunzi kwa ajili ya kujiunga na Program zetu ni kwa ngazi ya Shahada za awali kwa wale waliomaliza kidato cha nne, kidato cha Sita na hata waliomaliza muda mrefu,” amesema Dk.Eliza.

Amesema Chuo chao kina kampasi tatu ambazo zipo katika Mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam maeneo ya Upanga na Tegeta pamoja na mkoani Mbeya.

Katika ujenzi wa bweni DK.Eliza amewaomba Watanzania wakiwemo Wanafunzi waliomaliza Chuo hicho miaka ya nyuma (Alumni) kujitokeza na kuchangia kampeni ya ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi wa kike mkoani Mbeya ambapo Mkuu wa Mkoa ameuzindua ambapo Kuna namba maalumu ya kuchangia ambayo ni kupitia control namba 994180331310.

Hivyo amewakaribisha na amewaomba wananchi kwa ujumla kuchangia ujenzi wa hosteli za Wanachuo wa kike katika kampasi ya Mbeya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here