Home BUSINESS CHUO CHA BENKI KUU MWANZA CHAKARIBISHA WANAFUNZI MWAKA MPYA WA MASOMO

CHUO CHA BENKI KUU MWANZA CHAKARIBISHA WANAFUNZI MWAKA MPYA WA MASOMO

Mratibu wa Mafunzo Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania kilichopo Jijini Mwanza, Tulla Mwigune, akifafanua jambo alipokuwa akielezea kozi mbalimbali zinazotolewa kwenye Chuo hicho, kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mafunzo Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania cha Jijini Mwanza, Tulla Mwigune akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika Banda la Benki Kuu, kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Chuo cha Benki Kuu kilichopo Jjini Mwanza, kimeendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea Banda la Benki Kuu katika Maonesho ya Biashara ya 47 ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mafunzo Chuo cha Benk kuu Mwanza, Bi. Tulla Mwigune, amesema lengo la kuwa katika viwanja hivyo ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu Chuo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1991 kwa malengo hasa ya kutoa elimu kwa wafanyakazi wa Benki.

“Jinsi mafunzo hayo yalivyoenda tuliona kuna uhitaji pia wa kutoa elimu kwa wafanyakazi ambao wapo kwenye Taasisi za fedha ndani ya nchi, pamoja na nchi zilizopo katika ukanda wa Afrika Mashariki, na zilizopo kusini mwa Afrika.

“Ilipofika mwaka 2020 kupitia maoni ya wadau, Benki kuu ikaona ni vyema pia ianze kuwajenga vijana wanaotoka kidato cha sita. 

“Pia tunapokea wanafunzi waliomaliza kidato cha nne lakini awe na cheti cha maswala ya Biashara mfano, kama maswala ya Banking, Finance na Account, anaweza akajiunga na chuo chetu kwa masomo ya Diploma kwa miaka miwili” amesema Tulla.

Aidha ameeleza kuwa mwanafunzi wa masomo ya Diploma atatakiwa kutuma maombi yake moja kwa moja Chuoni kupitia mfumo wa Chuo hicho ambao ni: https://oas.botac.ac.tz. na kwamba, dirisha la Udahili bado liko wazi kwa awamu ya kwanza hadi Julai 28, mwaka huu, na baadae kufunguliwa tena mwezi Ogasti kwa awamu ya pili.

Chuo hicho kinatoa pia Programu za muda mfupi kwa watu waliopo katika taasisi za fedha. Lengo ni kuwapa ujuzi na kuongeza ufanisi wa utendaji wao wa kazi. Ratiba ya Programu hizo inatoka kila mwaka mwezi Novemba, na inapatikana katika website ya chuo ambayo ni academy.bot.go.tz.

Ameongeza kuwa Programu nyingine ni  Stashahada ya uzamili (Postgraduate Diploma in Bank Management), mafunzo hayo yanayoendeshwa katika vyumba vya mafunzo vilivyopo Benki Kuu makao makuu ndogo Dar es Salaaam.

Sifa za kujiunga na programu hii ni Shahada ya kwanza, yaani (Bachelor degree), au Stashahada ya juu (Advanced Diploma) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 September 2023 na masomo yataanza rasmi mwezi October 2023.

Previous articleCHUO KIKUU MZUMBE CHAPONGEZWA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA KAMPASI YA MBEYA
Next articleUWT ILALA WATOA TUZO KWA MWENYEKITI SAID SIDE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here