Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mbunge wa jimbo ka Mjini Mh. Mrisho Gambo katika. Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye iwanja wa Shekh Amri Abeid mkoani humo ambapo viongozi mbalimbali wametoa hotuba na kufafanua mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya uwekezaji hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na msanii Harmonize wakati alipotumbuiza katika. Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shekh Amri Abeid mkoani humo ambapo viongozi mbalimbali wametoa hotuba na kufafanua mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya uwekezaji hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amesema Chama kimeridhika na Utendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa Ilani.
Akizungumza Mkoani Arusha Ndugu Chongolo amesema kuwa utekelezaji wa Ilani imejenga matumaini makubwa kwa wananchi kutokana na upatikanaji wa huduma za kijamii.
Ndugu Chongolo amesema kuwa ilani ya CCM ilitoa ahadi na inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo huduma ya maji pamoja na miundombinu ya barabara.
Amesema kuwa katika Mkoa wa Arusha serikali imetoa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji.
“Mkoa wa Arusha, Manyara, Kilimanjaro kuna miradi mingi ya barabara inaendelea kutekelezwa katika Jiji la Arusha” amesema Ndugu Chongolo