Afisa Uhusiano wa Umma kutoka Idara ya Mawasiliano, Bi. Beatrice Ollotu, akizungumza kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw. Elirehema Msemembo, akitoa elimu kuhusu alama za usalama katika noti kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Tafiti na Sera za Uchumi, Bw. Elisha Mkandya, akifafanua jambo kwa mwananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Ujumuishi wa Fedha, Bw. Ramadhani Myonga, akielezea jambo kwa mwananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania, Bi.Tulla Mwigune, akifafanua jambo kuhusu Chuo cha BoT kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Helasita waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Benki kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bw. Andrea Chimbotela, akielezea jambo kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Benki Mkuu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Mwile Kauzeni
Mhasibu kutoka Bodi ya Bima ya Amana, Bi. Beatrice Kallanga, akifafanua jambo kwa mwananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Benki Mwandamizi, Bi. Rukia Muhaji.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inashiriki Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama SABASABA yanayofanyika viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni 2023 hadi 14 July 2023.
Katika Maonesho hayo BoT inatoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ambapo wananchi wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo sera za fedha, namna yakuwekaza katika dhamana za serikali, mifumo ya malipo ya taifa, namna BoT inasimamia sekta ya fedha nchini, utatuzi wa malalamiko ya mtumiaji wa huduma za kifedha, masuala ya ajira na utumishi Benki Kuu, nafasi za masomo katika Chuo cha BoT pamoja na Bodi ya Bima ya Amana. Pia, BoT inatoa elimu kuhusu utambuzi wa alama za usalama katika noti zetu nan jia sahihi za utunzaji wa noti na sarafu.