Home BUSINESS BoT YAFANYA KIKAO NA WAFANYABIASHARA WA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI...

BoT YAFANYA KIKAO NA WAFANYABIASHARA WA MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI (BUREAU DE CHANGE)

Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, akizunguzma leo Julai 17, 2023 wakati akifungua kikao cha majadiliano baina ya BoT na wafanyabiashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau de Change) kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyabiashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau de Change) wakiwa kwenye kikao hicho cha majadiliano na BoT Julai 17, 2023.

Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba akiongoza kikao hicho.

  Meneja Idara ya Mawasiliano BoT, Bi. Victoria Msina akitoa maelezo ya utangulizi wa kikao hicho.

Baadhi ya wafanyabiashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau de Change) wakiwa kwenye kikao hicho cha majadiliano na BoT Julai 17, 2023.

NA: KHALFAN SAID, K-VIS BLOG.

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imekutana na wafanyabiashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau de change) kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya kuwafikishia wananchi huduma hiyo wakati huu dunia inakabiliwa na uhaba wa dola ya Kimarekani.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho cha majadiliano, Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba amesema licha ya changamoto hiyo ya kidunia, Tanzania imeendelea kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni (kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kwa miezi isiyopungua minne).

Hata hivyo, alionya kuwa mafanikio hayo kamwe yasiwafanye (wasimamizi-BoT) na wafanyabiashara (watoa huduma) kubweteka na hiyo ndio sababu iliyoisukuma BoT kuitisha mkutano huo

Alisema Benki Kuu inafuatiliankwa ukaribu tatizo hilo la kidunia na imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana nalo.

Alisema katika kipindi cha matumizi ya Kanuni za Kubadilisha Fedha zan Kigeni za mwaka 2019, Benki Kuu imebaini changamoto kadhaa ambazo zimeathiri utoaji wa huduma hiyo nchini na kutaja miongoni mwa changamoto hizo ni wawekezaji wengi kushindwa kukidhi matakwa ya Kanuni, hususan mtaji wa shilingi bilioni 1, hivyo kusababisha kuwepo kwa watoa huduma wachache.

“Hali hii imepelekea upatikanaji hafifu au kukosekana kwa huduma hii katika baadhi ya maeneo yenye uhitaji huo,” alibainisha Gavana Tutuba.

Alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo, Benki Kuu ilifanya mkutano na wadau wa biashara ya kubadilisha fedha za kigeni nchini mwezi Januari na Aprili 2023 ili kupata maoni ya namna ya kuboresha mazingira ya biashara hiyo.

“Kumekuwepo na maoni mbalimbali, wapo wanaosema sharti la mtaji liwe shilingi Milioni 500, lakini wapo pia wanaosema hata shilingi Milioni 200 wanaweza kufanya baishara hiyo, sasa haya yote tuyaajadili hapa.” Alisema.

Vilevile, Benki Kuu kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikutana na wadau wa sekta ya hoteli Zanzibar mnamo mwezi Januari 2023 na kujadili namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni katika maeneo ya hoteli za kitalii.

Alisema baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali, Benki Kuu ilianzisha mchakato wa kupitia upya Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za 2019 kwa lengo la kurekebisha baadhi ya masharti ili wawekezaji wengi zaidi waweze kuhamasika kuanzisha biashara hiyo na wale waliokuwepo waweze kurejea katika biashara hii.

“Marekebisho haya yanajumuisha kupunguza kiwango cha mtaji ili kuwawezesha wawekezaji wengi wazawa kufungua maduka mapya ya kubadilisha fedha za kigeni.

Aidha, Kanuni mpya zinalenga kuweka utaratibu utakaowezesha hoteli za kitalii nchini kutoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kwa wateja wao.” Alifafanua Gavana Tutuba.

Hatua nyingine ambazo BoT imechukua kukabiliana na uhaba wa dola ya Marekani duniani ni pamoja na kuweka mikakati mizuri ya kupunguza uagizaji bidhaa kutoka nje kwa kuonegza thamani na ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini.

“Katika hili Benki Kuu itatoa udhamini kwa mfanyabiashara anayehitaji kukopa fedha kwenye benki ya kumuwezesha kuongeza ubora na tahamani ya bidahaa zinazozalishwa nchini ili watanzania washawishike kununua bidhaa hizo hapa hapa nyumbani badala ya kuagiza kutoka nje.”Alifafanua.

Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, akizunguzma leo Julai 17, 2023 wakati akifungua kikao cha majadiliano baina ya BoT na wafanyabiashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau de Change) kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyabiashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau de Change) wakiwa kwenye kikao hicho cha majadiliano na BoT Julai 17, 2023.

Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba akiongoza kikao hicho.
Meneja Idara ya Mawasiliano BoT, Bi. Victoria Msina akitoa maelezo ya utangulizi wa kikao hicho.

Baadhi ya wafanyabiashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni (Bureau de Change) wakiwa kwenye kikao hicho cha majadiliano na BoT Julai 17, 2023.

CREDIT: K-VIS BLOG.

Previous articleWATUMISHI BRELA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA MSHIKAMANO
Next articleUDOM YASHIRIKI MAONESHO YA VYUO VIKUU MNAZI MMOJA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here