Home LOCAL DANIEL CHONGOLO KUUNGURUMA DAR ES SALAAM

DANIEL CHONGOLO KUUNGURUMA DAR ES SALAAM

Na: Heri Shaaban (Ilala)

KATIBU Mluu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa Daniel Chongolo, anatarajia kuunguruma Mkoa Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Wilayani Kinondoni kuongea na Wananchi Ili kuwaelezea Watanzania kwa kina dhamira ya dhati ya ccm kuwaletea Maendeleo Watanzania .

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM mkoa Dar es Salaam Abbas Mtemvu, alisema Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo ,anatarajia kufanya mkutano mkubwa katika Kanda Dar es Salaam mara baada kumaliza ziara zake katika mikoa mbalimbali .

“Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo atakuwa na mkutano mkubwa mkoa Dar Es Salaam siku ya Jumamosi Julai 29/2023.

kwa ajili ya kuelezea kazi kubwa zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt ,Samia Suluhu Hasan, ikiwemo Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi wa Mkoa Dar Ea Salaam mjitokeze mpate fursa ya kuyasikia mengi ya Maendeleo ambayo yanatekelezwa katika Ilani ya Chama Cha mapinduzi CCM ” alisema Mtemvu

Mwenyekiti Mtemvu alisema katika mkutano huo mkubwa wananchi wataelezwa yanayotarajia kufanyika na yalio katika mkakati na malengo ya CCM kwa Jiji la Dar es Salaam.

Alisema katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM 2020 /2025 yapo mengi yamepangwa ya Maendeleo namna gani na lini CCM inaenda kuyaanzisha ambayo hayajaanza na kuyakamilisha yalioanzishwa na Serikali ya awamu ya sita .

Aidha alisema katika mkutano huo vikundi mbali mbali vya Burudani za wasanii pia kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kufanya biashara zao kwani mambo hayo yanapatikana CCM peke yake .

Alitoa wito kwa Wananchi ,Jamaa ,wadau ,wakereketwa na Wananchi wote wenye mapenzi mema na CCM tushirikiane kwa pamoja kufanikisha nia njema ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa ya kuhakikisha kwa asilimia kubwa Wananchi wa Mkoa Dar es Salaam wanaenda kusikiliza dhamira ya ccm ya kuwaletea Maendeleo .

Alitumia fursa hiyo pia kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa CCM Tanzania kwa namna anavyosimamia Serikali vizuri na kuwetea Wananchi Maendeleo katika Mkoa huo ambapo Wananchi wote mashahidi kazi kubwa inayofanyika katika sekta Elimu ,Afya ,Barabara ,Maji ,umeme ,biashara ,Uwezeshaji,wa Wananchi kiuchumi ambapo matunda hayo yanaendelea kustawisha jiji hilo .

Katibu Mkuu Daniel Chongolo alianza ziara yake katika mikoa mbalimbali Ikiwemo Mbeya,Singida Arusha,Mtwara,Kigoma ,ambapo Sasa hivi Mkoa Dar es Salaam
Mwisho

Previous articleRAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA DODOMA
Next articleSIWANI, MBUNGE ASIYEFANYAKAZI HAFAI KUWA KIONGOZI – MTEMVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here