Home LOCAL WAZIRI UMMY MWALIMU AWAPA MAUA YAO (SIFA) DKT.YOTI NA BI.SHALINI

WAZIRI UMMY MWALIMU AWAPA MAUA YAO (SIFA) DKT.YOTI NA BI.SHALINI

Na: Mwandishi wetu – WAF.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo ameagana rasmi na kuwapa pongezi zao Mwakilishi wa UNICEF Bi. Shalini Bahuguna pamoja na Mwakilishi Mkazi wa WHO Dkt. Zablon Yoti aliyewakilishwa na Bw. Maximilian Mapunda ambao walimaliza muda wao wa kutumikia nafasi hizo hapa Nchini.

Waziri Ummy ametoa pongezi hizo mapema Leo katika hafla fupi ya kuwaaga viongozi hao katika ukumbi wa Serena Hotel, jijini Dar es Salaam.

“Nawashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi nzuri mliyoifanya hapa nchini kwa kuendelea kuimarisha mifumo katika sekta ya Afya hususani maeneo ya upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo kwa watoto na masuala ya usafi na lishe”. Amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Bi. Shalini Bahuguna ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye mashirika ya kimataifa ikiwemo UNICEF NA WHO.

Naye Bw. Maximilian Mapunda aliyemuwakilisha Mwakilishi mkazi wa WHO Dkt. Zablon Yoti ameiwashukuru Wizara ya Afya kwa ushirikiano walioutoa wakati wa muda wake na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 102023
Next articleBENKI YA CRDB YAKABIDHI GAWIO KUBWA ZAIDI KUPATA KUTOKEA LA SHILINGI BILIONI 45.8 KWA SERIKALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here