Home BUSINESS TUWAJBIKE KULIPA KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU – TRA 

TUWAJBIKE KULIPA KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU – TRA 

NA MWANDISHI WETU 

Hii ni kauli mbiu ya  Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA)  kwa mwaka 2023 kupitia kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo. 

Akifungua semina ya wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Jiji la Dar es Salaam (DCPC) wiki iliyopita, Kayombo alisema kila Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18, anao wajibu wa kulipa kodi kwa maendeleo na ustawi wa Taifa.  

Katika semina hiyo maalum kwa ajili ya kuwakumbusha wanahabari mambo mbalimbali kuhusu elimu ya mlipa kodi nchini, Kayombo alisema Watanzania lazima watambue maendeleo yote wanayoyaona yakifanyika yanatokana na kodi inayokusanywa na TRA. 

Aidha Kayombo alisema bila kulipa na kukusanya kodi, Tanzania inaweza kuangamia kwa sababu maendeleo yote yaliyopo na yahayo yanategemea kodi.  

“Haya maendeleo tunayoyaona hayaji kimiujizi bali ni kodi zinazolipwa na kukusanywa.”alisema Kayombo huku akisisitiza kuwa hakuna maendeleo yoyote yanayopatika kwenye Taifa lolote bila wananchi wake kulipa kodi.  

Mkurugenzi huyo pia alitoa wito kwa Watanzania kuwa na desturi ya kupenda kulipa kodi.  

Naye Ofisa Mkuu wa  Usimamizi wa Kodi wa TRA, Hamad Mterry wakati akitoa mada ya elimu kwa mlipa kodi kwenye semina suala la kodi ni kama kifo kwani halikwepeki. 

“Kama ambavyo binadamu hatuwezi kukwepa kifo vivyo hivyo na kodi haikwepeki kwa namna yoyote kwakuwa inalipwa kwa namna mbalimbali. 

Mterry pia alizungumzia mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2022 ambayo yameweka ukomo hadi kufikia Desemba mwaka huu 2023 kila mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18,  awe amejisajili na kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN). 

“Kwa utaratibu huu, kuanzia Decemba 2023 itakuwa ni kosa la jinai iwapo Mtanzania mwenye umri wa miaka kuanzia 18 hatokuwa na TIN isiyo ya kibiashara” alisema.  

Mterry pia alisisitiza kuwa TIN ni jambo la muhimu mno kwa sababu  inahitajika pindi mtu akitaka kufanya malipo mbalimbali ikiwamo kulipia leseni ya udereva, leseni ya biashara, kulipia masomo ya juu,  matibabu n.k. 

Mteri akifafanua zaidi kuwa kujisajili kuwa mlipa kodi hakuna malipo yoyote na kwamba TRA imerahisisha zaidi utaratibu huo kwani, mtu atajisajili kwa njia ya kidigitali kutokea mahali popote alipo. 

“Mtu au taasisi, inatakiwa kuwa na TIN moja tu, na hiyo hiyo  itakuwa inatumika kwa matumizi yote iwe kibiashara au binafsi.” Alisema Mterry. 

Mwisho 

Previous articleYANGA SC YAANDIKA HISTORIA SOKA LA AFRIKA
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 13, 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here