Na: Heri Shaaban (Ilala)
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila, ametoa onyo kwa Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam kuacha kupokea Bahasha badala yake amewataka wakazane kukusanya mapato ya Halmashauri ,Diwani au Mtendaji wa Halmashauri hiyo akitiwa bahasha atoe taarifa mkoani ili aweze kupewa mara mbili ya bahasha .
Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila ,alitoa onyo hilo kwa Madiwani wa hamashauri hiyo na Watendaji wakati wa Baraza la Madiwani walipokuwa wakiwasilisha taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu za Serikali ( CAG) ambapo Halmashauri hiyo imepata hati safi kwa miaka saba mfululizo kuanzia mwaka 2015 mpaka mwaka 2022
“Naipongeza Ilala kwa hati safi nawagiza Madiwani na Watendaji kufanya kazi kwa weledi na kuziba hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali CAG zisijitokeze tena hoja zilizojotokeza zizibwe kwa wakati kutokana na Watumishi kushindwa kusimamia Majukumu yao ipawavyo “ alisema Chalamila .
Mkuu wa Mkoa Chalamila alisema mchezo wanaofanya watu wa kitengo cha mapato cha ukusanyaji huduma za Halmashauri msipowasimamia vizuri Mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya nitawachukulia hatua.
Aliwataka wafanye kazi kwa weledi bila kuoneana aibu Ili kuweza kukusanya mapato ya serikali vizuri iweze kifikia malengo wasioneane aibu kwa ajili ya mgao wanaopata na kuwataka Madiwani na Watendaji kuwafichua masuala ya kuchukua Bahasha ikitokea suala la mgao wa Bahasha watoe taarifa Ofisi ya mkoa waweze kupewa Bahasha mara mbili
Aidha Chalamila alisema anafahamu mnyororo wa Kampuni ya ukamataji magari ambao unadaiwa kufanya kazi usiku za ukamataji makontena bila kuingizwa katika mapato ya Serikali posi mashine
Katika hatua nyingine alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kusimamia vizuri kitengo cha Mkaguzi wa ndani kwani ni sehemu muhimu kabla suala kufika kwa CAG lazima mambo yote ya Halmashauri yaanzie hapo
Aliwagiza Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa usahihi Ili kuisaidia Serikali katika suala la ukusanyaji mapato.
Mwisho.