Na Heri Shaaban (Ilala)
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuwaondoa watumishi wa Halmashauri hiyo watakaoshindwa kusimamia mapato ya serikali vizuri.
Mkuu wa Mkoa Chalamila alisema hayo katika ziara wilayani Ilala wakati wa kukagua miradi ya Maendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
“Nakuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam simamia mapato ya serikali vizuri na Watumishi wako ,waondoe Watendaji wanaoiba mapato ya serikali “ alisema Chalamila .
Mkuu wa Mkoa Chalamila akizungumzia ziara ya kukagua miradi Wilaya ya Ilala alimwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jomaary Mrisho kuzuia mwendelezo wowote wa ujenzi katika shule ya Msingi Kivule Mpya iliyopo Magole badala yake Serikali ikitoa pesa eneo lililobaki wajenge shule ya gholofa kutokana na idadi kubwa ya Wananchi wa eneo hilo na shule zilizopo chache
Chalamila aliwataka wananchi na Wazazi kutoa ushirikiano na Serikali kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa kuunga mkono Juhudi za maendeleo Serikali itawasogezea huduma za kijamii karibu na makazi yao ikiwemo kuwajengea Miundombinu ya Barabara kwa kiwango cha lami ,masoko na sekta ya Elimu na Afya.
Akizungumzia mradi wa shule ya sekondari Kata ya Liwiti alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kuelekeza fedha nyingi katika sekta ya Elimu ambapo Kata ya Liwiti kupitia pochi la mama wameweza kujenga sekondari ya gholofa yenye madarasa 20 ambayo yanatarajia kutumika hivi karibuni .
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, alisema Kata ya Liwiti ndio shule ya kwanza ya Serikali ambayo imejengwa ya kisasa katika utekekezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi .
Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Saidi Side alisema kilio cha wakazi wa Liwiti kimepata ufumbuzi wake kiu yao kubwa ilikuwa shule ya Serikali za imepatikana Wazazi sasa wajipange kupeleka Watoto kusoma karibu na Makazi yao .
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo aliwapongeza kwa ushirikiano wao Ilala ngazi ya chama na Serikali wanafanya KAZI kubwa kuanzia Mwenyekiti wa çcm Wilaya ya Ilala Said Sidde Meya wa halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto na madiwani wa Halmashauri wanashirikiana katika kujenga serikali .
Mwisho