Home BUSINESS RC CHALAMILA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SOKO LA KIGOGO FRESH-CHANIKA

RC CHALAMILA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SOKO LA KIGOGO FRESH-CHANIKA

 

– Akuta mazingira yasiyoridhisha ya kufanyia biashara

– Apokea kero mbalimbali kutoka kwa wafanyabishara wa Soko hilo

– Awataka kumpa muda ndani ya wiki moja kuanzia leo Juni 8,2023 kuzipatia ufumbuzi

DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 8, 2023 amefanya ziara ya kushtukiza katika Soko la Kigogo Fresh Chanika Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika Soko hilo amejionea mazingira yasiyoridhisha katika Soko hilo ambapo hata barabara ya kuingia sokoni hapo imejaa maji hali ambayo husababisha jamii inayofuata mahitaji sokoni hapo na wafanyabishara wanafanya biashara kupata shida hasa nyakati za mvua

Aidha RC Chalamila alipata wasaa wa kuongea na wafanyabishara hao wakimueleza kero mbalimbali zinazowakabili sokoni hapo ikiwemo miundo mbinu mibovu ambapo amewaambia tayari fedha zilishaletwa katika soko hilo hivyo ndani ya Kipindi kifupi kuanzia sasa Changamoto zote zitaisha.

Huku akiwataka kumpa muda wa wiki moja kuanzia leo kuzishughulikia Changamoto hizo, Mhe Chalamila amesema atapita kila mahali kushughulikia Changamoto za wana Dar es Salaam hataki kupewa taarifa za makaratasi Ofisini.

Sambamba na hilo RC Chalamila amesema Rais Samia Suluhu hapendi mtu yoyote anyanyasike Serikali inategemea mapato kutoka kwa wafanyabishara hivyo lazima tuboreshe mazingira yao ya kufanyia biashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here