Home LOCAL MIRADI YENYE MAJINA MAZURI ISIYO NA TIJA HAINA MAANA – CHONGOLO

MIRADI YENYE MAJINA MAZURI ISIYO NA TIJA HAINA MAANA – CHONGOLO

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ameigiza Wizara ya Kilimo kukaa na Wizara ya Fedha kukutana na kujadili namna ya kuendeleza miradi ya kilimo ili imalizike ndani ya muda mfupi.

Chongolo ametoa agizo hilo alipotembelea mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Jenga Kesho Bora uliopo Chinangali Wilaya ya Chamwino.

Amesema dhamira ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan ni kuona miradi ya kilimo inaleta tija kwa haraka,hivyo haileti maana kuona kuna miradi yenye majina mazuri lakini haina tija kwa wananchi.

Mradi wa Jenga Kesho iliyo bora – BBT ni miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo inayowalenga vijana,ambapo katika Ziara yake akiwa katika Wilaya ya Kongwa,aliagiza miradi hiyo ikamilike kufika mwezi Agosti mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here