Home BUSINESS TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MFUMO MPYA WA UTEKELEZAJI WA SERA YA FEDHA...

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MFUMO MPYA WA UTEKELEZAJI WA SERA YA FEDHA KWA KUTUMIA RIBA ZA BENKI KUU

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa katika jitihada za kuboresha ufanisi wa  utekelezaji wa sera ya fedha, inatarajia kubadilisha mfumo wa sasa wa utekelezaji wa sera ya  fedha, ambao unatumia ujazi wa fedha, na kuanza kutumia mfumo mpya unaotumia riba ya  Benki Kuu (Central Bank Policy Rate) katika kusimamia malengo mapana ya kiuchumi ya  kudumisha utulivu wa bei na ukuaji wa uchumi kuanzia mwezi Januari 2024. Mfumo huu ulianza  kutumika duniani mwaka 1990 ambapo hadi sasa unatumiwa na Benki Kuu za nchi 45.  

Utekelezaji wa Mfumo wa Riba ya Benki Kuu umeonesha matokeo mazuri katika usimamizi wa  sera ya fedha na kuimarisha misingi ya utekelezaji wake katika mazingira ya uwazi katika nchi  zinazotumia mfumo huu. Maelezo na ufafanuzi zaidi kuhusu mfumo huu mpya wa sera ya fedha  yameambatishwa na taarifa hii kama Kiambatisho Na. I. Aidha, maelezo ya ziada yanapatikana  pia katika Tamko la Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania ya 2023/24 na Tovuti ya Benki Kuu  ya Tanzania: www.bot.go.tz/Publications/Filter/48?lang=sw 

Kwa muktadha huu, ili kuhakikisha kuwa mabadiliko haya yanafanyika kwa ufanisi, Benki Kuu  ya Tanzania imeandaa Mwongozo wa utekelezaji wa sera ya fedha kwa kutumia riba ya Benki  Kuu ambao umeambatishwa na taarifa hii kama Kiambatisho Na. II. Madhumuni ya Mwongozo  huu ni kutoa taarifa muhimu kwa wadau ili kuongeza uelewa kuhusu sera ya fedha, hatua na  taratibu zinazohusika katika mfumo mpya wa sera ya fedha kwa kutumia riba. Mwongozo huu  utasaidia kutoa ufafanuzi kuhusu uandaaji na utekelezaji wa sera ya fedha ili kuwezesha wadau  kupangilia shughuli zao na kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa sera ya fedha.  

Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kushirikisha wadau mbalimbali kwa lengo la kuongeza uelewa  juu ya mfumo mpya wa sera ya fedha na hivyo kuwezesha kufikia malengo ya sera ya fedha ya  kudumisha utulivu wa bei na kusaidia ukuaji endelevu wa uchumi. 

GAVANA 

BENKI KUU YA TANZANIA 

  

Previous articleMGODI WA BUCKREEF WAWAJENGEA UWEZO WAJASIRIAMALI WANAWAKE WILAYA YA GEITA
Next articleWAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA WATENDAJI WA HALMASHAURI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here