Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalamu wa Alsalam Internatinal Hospital ya nchini Misri, imefanya kambi ya upasuaji wa kupitia matundu madogo (Laparoscopy surgery) kwa muda wa siku mbili ambapo kina mama watano wamenufaika na matibabu hayo.
Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo leo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Upasuaji wa Matundu Madogo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Vincent Tarimo amesema waliofanyiwa upasuaji huo wengi walikuwa na changamoto ya uvimbe kwenye kizazi.
“Upasuaji wa matundu madogo hufanyika kwa kutoboa sehemu ndogo ya mwili kwa kuingiza vifaa maalumu ambapo una faida nyingi kwa kuwa mgonjwa hapati majeraha makubwa na uvujaji wa damu hivyo kupona haraka ili kuendelea na shughuli zake baada ya muda mfupi” amesema Dkt. Tarimo.