Home BUSINESS iSOKO YALETA NEEMA YA BIASHARA KIDIJITALI 

iSOKO YALETA NEEMA YA BIASHARA KIDIJITALI 

Wanawake Changamkieni Fursa za Biashara Kidijitali

Wajasiriamali nchini wametakiwa kufanya biashara zao kisasa ili kuendana na teknolojia huku wakiaswa kuwa waaminifu Kwa wateja wao.

Wito huo umetolewa Mei 24, 2023 na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Needpeace Wambuya wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kidigital wa biashara Kwa wafanyabiashara wanawake (isoko), amesema kuwa uwepo wa mfumo huo utasaidia upatikanaji wa masoko Kwa urahisi hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuteka soko la Afrika Mashariki.

Aidha Wambuya ameongeza kuwa serikali imeweka mazingira mazuri Kwa wafanyabiashara hivyo wanapaswa kuboresha biashara zao na kuwa wazalendo Kwa kulipa Kodi stahiki ili kukuza na kuinua uchumi wa nchi.

“Serikali yetu imejitahidi kuweka mazingira mazuri Kwa wafanyabiashara hivyo basi nitoe rai kwenu wajasiriamali kuingia kwenye mfumo huu wa Isoko ili mtangaze bidhaa zenu Kwani kufanya hivyo mtakua mnaitangaza nchi na kuinua uchumi wetu,” amesema Wambuya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wanawake (TWCC) Mercy Sila ametoa rai kwa wafanyabiashara kutengeneza bidhaa zinazokubalika sokoni Kwani soko la Tanzania kwa sasa limekua na serikali imeweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara.

Aidha Sila ameongeza kuwa TWCC ina zaidi ya wanawawake elfu 10000 ambao wanafanya nao kazi hivyo anaamini kupitia mfumo wa iSoko utasaidia kukuza na kuinua vipato vya wanawake hao na kujitangaza na kuzitangaza bidhaa zao kimataifa

Naye Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Afrika Nchini Tanzania Monica Hangi amesema kuwa wajasiriamali wanapaswa kuthubutu hata kama mitaji yao ni midogo kwani hii ni fursa kwao hivyo wanapaswa kuongeza uaminifu na kuboresha bidhaa.

“Hii forum ni fursa kwenu wajasiriamali kujitangaza lakini hakikisheni mnatangaza bidhaa nzuri na zenye viwango msitangaze bidhaa ghafi hii itasaidia kuitangaza nchi yetu na kujitangaza wenyewe pia kwani mfumo huu haujamuacha mfanyabiashara yoyote hata kama unatumia simu mdogo,” amesema Hangi.

isoko ni mfumo wa kigitali wa biashara Kwa wafanyabiashara wanawake lengo likiwa kuwanufaisha wajasiriamali kujitangaza na kutangaza bidhaa zao.    

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here