Home LOCAL CHONGOLO AKEMEA TABIA YA WIZI WA VIFAA VYA UJENZI MRADI WA RING...

CHONGOLO AKEMEA TABIA YA WIZI WA VIFAA VYA UJENZI MRADI WA RING ROAD DODOMA

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akipewa taarifa fupi kuhusu ujenzi mradi wa barabara ya Ring Road ya kilometa 112.3 ambayo inagharimu Sh.bilioni 220

 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akizungumza mbele ya wananchi (hawapo pichani) wanaozunguka pembezoni mwa ujenzi wa mradi wa barabara ya Ring Road ya kilometa 112.3 ambayo inagharimu Sh.bilioni 220, akiwaonya kuacha wizi na udokozi wa vifaa vinavyotumika kwenye mradi huo.

Muonekano wa barabara ianyoendelea kujengwa .Katibu Mkuu wa CCM Komredi Daniel Chongolo akipewa maelezo namna udongo unavyopimwa alipotembelea maabara ya kupima udongo kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Ring Road ya kilometa 112.3 ambayo inagharimu Sh.bilioni 220.Sampo ya udongo ambao unaendelea kupimwa kwenye maabara hiyo maalum ya kupimia udongo.

Na: Mwandishi wa Michuzi TV – Dodoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewaonya wananchi wanaozunguka pembezoni mwa ujenzi wa mradi wa barabara ya Ring Road ya kilometa 112.3 ambayo inagharimu Sh.bilioni 220 kuacha wizi na udokozi wa vifaa vinavyotumika kwenye mradi huo.

Amesema wizi wa vifaa unaofanyika kwenye mradi huo madhara yake yanakwenda katika Serikali kwasababu ndio inayokwenda kufidia gharama za ule wizi unaotokea kwa wakandarasi ,hivyo wajiepushe na vitendo vya wizi.

Akizungumza leo baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Ring Road eneo la Nala, Chongolo pamoja na mambo mengine amesema wanaojihusisha na wizi wa vifaa vya ujenzi ni kosa kisheria lakini wanahujumu uchumi wetu wenyewe kwasababu wanajiibia kukwamisha maendeleo yetu wenyewe.

“Tuache tabia ya wizi ,tabia ya tama ya kupenda vitu ambavyo sio halali na ambavyo hatuvipati kwa jasho, tufanye kazi ili tupate vilivyo halali,”amesema Chongolo huku akitumia nafasi hiyo kupongeza kasi ya mradi pamoja na ubora.

“Uzuri sisi wengine tumekuwa tunaona hii miradi kwa hiyo nilivyoona tu unaona kabisa viwango vimezingatiwa lakini pia na uamuzi wa kuweka kuwa njia nne zenye barabara mbili zinazotumika kupitia huo ni uamuzi wa busara na wa maana kwa Jiji letu la Dodoma.

Akiizungumzia kwa kina barabara hiyo ya mchepuko amesema inatija kubwa kwa maendeleo ya Dodoma na itafungua fursa kwa jiji la Dodoma kwani Ring Road hiyo inakwenda kufungua maendeleo ya uchumi kwa Jiji hilo.

Aidha amesema sasa ni wakati muafaka wa kutengeneza barabara ambazo zitakuwa zinatoka kwenye Ring Road kuingia kwenye makazi ya wananchi kuanzia kwenye mipango ya Jiji na kwenda TARURA na TANROADS wenyewe.

“Kikubwa kinachofurahisha kwenye mradi huu ni kuwa na kipengele kinachozungumzia kusogeza huduma kwa wananchi ,wametuambia hapa kupitia huu mradi kutakuwa na vituo vya afya vinne ambavyo vitakuwa vimekamilika.

“Kutakuwa na shule ya msingi kule Ihumwa pamoja na mambo mengine ya msingi yakiwemo visima vya maji vitakavyokwenda kuhudumia wananchi walioko pembezoni mwa mradi, haya ndio mafanikio.

Aidha amesema uamuzi wa kujengwa barabara hiyo inaonesha dhamira ya mapenzi ya Serikali lakini na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Jiji la Dodoma, na katika kurudisha mapenzi hayo ni vema wananchi wakafanya kazi kwa bidii ili kuchangia maendeleo ya nchi yetu , lakini kuchangia maendeleo ya Jiji la Dodoma.

Pia ametoa rai kwa wananchi kuacha kuvamia maeneo kiholela ili kuepukana na migogoro isiyo na sababu wala tija na mahali ambako miradi hiyo inapita waache kutengeneza hadithi za kujichongea laini za kujinufaisha hata kama sio sehemu halali.

CREDIT: Mchuzi Blog.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here