Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo uliofanyika Uwanja wa Mwembe Togwa Mjini Iringa, Chongolo amesisitiza kuwa CCM itaendelea kuisimamia serikali ili itekeleze mambo mbalimbali yaliyoainishwa kwenye Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025.
Pamoja na mambo mengine, Chongolo, amesema changamoto katika sekta ya Miundombinu, Kilimo, Maji, Afya na Elimu, zinatafutiwa ufumbuzi wa kina katika Mkoa wa Iringa kupitia kwa Mawaziri husika.
Mapema leo asubuhi, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa, Katibu Mkuu huyo wa CCM, amesema kukamilika kwake kutaleta faida kwenye kufungua Utalii na kurahisisha mawasiliano na usafiri katika Ukanda wa nyanda za Juu Kusini.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Chongolo, aliambatana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ambao ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Sofia Mjema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akifuatilia na kusikiliza kwa Makini kinachoendelea katika Mkutano wa kuhitimisha Ziara yake ya Siku 7 mkoani Iringa.
Pichani Juu ni Baadhi ya Mawaziri na Naibu Waziri wakizungumza na Kujibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Katibu Mkuu wa (CCM) Daniel Chongolo kutoka kwa Wananchi wakati wa Ziara yake ya Siku 7 mkoani Iringa.