Home BUSINESS BRELA YAWAPIGA MSASA MABENKI KANUNI ZA WAMILIKI MANUFAA

BRELA YAWAPIGA MSASA MABENKI KANUNI ZA WAMILIKI MANUFAA

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Isdor Nkindi, Akizungumza katika Warsha  ya Uhamasishaji wadau kuhusu Kanuni za wamiliki manufaa iliyofanyika mapema leo Juni 27, 2023, katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Andrew Mkapa akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Godfrey Nyaisa, alipokuwa akitoa hotuba ya utangulizi akimkaribisha Mgeni rasmi kufungua Warsha hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, akizungumza alipokuwa akifungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Benki Tanzania (TBA), Bi. Tuse Joune Akizungumza alipokuwa akihojiwa na waandishi wa Habari katika Warsha hiyo.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni za Biashara (BRELA) imeendesha Warsha ya Uhamasishaji wadau kuhusu Kanuni za wamiliki manufaa kwa kushirikiana na Umoja wa Benki Tanzania (TBA) kwa lengo la kutoa elimu juu ya mabadiliko ya Sheria ili kuweza kupata uelewa wa pamoja.

Akizungumza katika Warsha hiyo iliyofanyika mapema leo Juni 27, 2023, Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Usajili usajiri wa Kampuni na Majina ya Biashara (BRELA) Bw. Isdor Nkindi, amesema umiliki manufaa ni dhana mpya ambayo haikuwepo hapo awali Tanzania, na kwamba imekuja kufanya Kampuni zilizosajiliwa nchini ziweze kuwasilisha wahusika halisi ambao mwisho wa siku watanufaika na uendeshaji wa Kampuni hiyo.

“Tumekutana na Taasisi za kifedha ili kukumbushana na kuelimishana juu ya mabadiliko ya Sheria ili kuweza kupata uelewa wa pamoja. Mwaka 2020 tulifanya marekebisho mbalimbali lakini mojawapo ni kuongeza kipengele Cha kitu kinaitwa umiliki manufaa katika Kampuni.

“Umiliki manufaa ni dhana mpya ambayo haikuwepo hapo awali hapa nchini, hii imekuja kufanya Kampuni zilizosajiliwa hapa ndani ya nchi ziweze kuwasilisha wale watu ambao lazima wawe ni mtu halisi ambaye mwisho wa siku atanufaika na uendeshaji wa Kampuni,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Benki Tanzania (TBA), Bi. Tuse Joune amesema, anawashukuru Brela kwa kuandaa Warsha hiyo ambayo itawaelimisha kuhusu Sheria hiyo.

“Warsha hii ni sehemu mojawapo ya kutupa mwanga wenye Mabenki ili tuweze kuelewa utekelezaji wa Sheria hiyo ambayo inawahitaji Mabenki kama mmoja wa mtoa taarifa za mtumia huduma za kifedha ili kuelewa ni kwa kiwango gani au ni jinsi gani anatakiwa kujua taarifa au kutafuta taarifa za mmiliki wa mwisho, au mtoa maamuzi wa mwisho wa Kampuni.

Kwa upande wa Mabenki hii ni Semina muhimu sana kwa sababu ni Sheria ambayo utawekwa kama muongozo, kwa hiyo naamini wote mnaelewa kwamba kwa Benki moja ya jukumu letu ni kuhakikisha tunasimamia Sheria za nchi na kuzitekeleza” amesema Bi. Tuse.

Awali akizungumza alipokuwa akifungua Warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ameishukuru Brela kwa kuichagua Ilala hiyo kuwa mwenyeji wao kwa kuwa Ilala ndio kitovu cha Biashara katika Jiji la Dar es Salaam.

“Warsha hii ambayo Brela imefanya kwa niaba ya Serikali ni jambo kubwa katika mabadiliko ya Sheria ambazo zinaruhusu maswala ya Kampuni Bunge letu limepitisha mswaada wa Sheria ambao unahusika na maswala ya fedha na lengo kubwa kupitisha na kubadilisha Sheria hii sura ya namba 212,ilikuwa ni kupata za wamiliki.

“Changamoto za taarifa za wamiliki ni kwamba watu wengi walikuwa wanatumia makampuni kukwepa Kodi lakini wengi walikuwa wanatumia makampuni kupitisha fedha haramu,na wengi walikuwa wakipitisha fedha hizo haramu kupitia mabenki kwa hiyo kwa warsha hii itakwenda kutatua changamoto hizo,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here