Home SPORTS YANGA YAFUZU NUSU FAINALI SHIRIKISHO

YANGA YAFUZU NUSU FAINALI SHIRIKISHO

NA: TIMA SULTAN

LICHA ya kubanwa mbavu na kuambulia suluhu mbele ya wapinzani wao Rivers United leo Jumapili lakini jambo hilo halikuweza kuwazuia Yanga kuweza kuweka rekodi yao ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwenye Dimba la Benjamini Mkapa, Dar walijikuta wakikumbana na upinzani wa juu kutoka kwa wapinzani wao Rivers United ambapo ushindi wao wa awali wa mabao 2-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza nchini Nigeria uliweza kuwabeba na kufanikiwa kusonga mbele katika hatua hiyo ya nusu fainali.

Kwenye mchezo huo Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa ya nyota wake akiwatumia baadhi ya wachezaji ambao hawakuwa wanaanza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kutokana na matokeo ya mechi ya kwanza kuwabeba.

Katika mchezo huo dakika ya 25, mchezo ulisimama kwa muda kutokana na hitilafu ya umeme kabla mambo kukaa sawa na mchezo kuendelea.

Kwenye hatua ya nusu fainali Yanga wanakwenda kukutana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambayo ilishinda kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Pyramids yaa Misri, kwa kuwa robo fainali ya kwanza walitoshana nguvu wa kufungana bao 1-1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here