Home SPORTS YANGA SC IMARA KUIVAA MALLUMO ‘OUR TIME OUR TEAM’

YANGA SC IMARA KUIVAA MALLUMO ‘OUR TIME OUR TEAM’

NA: TIMA SULTAN

KUEKELEKEA Kwenye Mchezo wao wa Nusufainali Kombe la shirikisho la Afrika unaotarajia kuchezwa May 10, Uongozi wa Yanga umesema kauli mbiu yao ni ‘OUR TEAM OUR TIME’.

Yanga May 10 watashuka kwenye Dimba la Benjamini Mkapa, Jijini Dar es Salaam dhidi ya Mallumo Gallants ya kutoka Afrika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel, Msemaji wa klabu hiyo Ally Kamwe, aliwaita mashabiki wao kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa huku akitamba kuwa kauli mbiu yao kuelekea kwenye mchezo huo ni ‘Our Team Our Time’

Amesema mashandano hayo ya kimataifa hayana timu dhaifu nimfupa mgumu sana lakini anaamini kwamba fainali za mashindano hayo zitawafikia lakini wanahitaji mtaji mkubwa wa mashabiki wao

“Timu tuliyopangiwa sio rahisi kama ambavyo watu wanafikiria chamuhimu nimashabiki kujitokeza kuja kuongeza morali uwanjani kwa wachezaji wetu,” alisema

Amesema pia kuna kauli mbiu yakipekee kuelekea kwenye mchezo huo mkubwa wa historia kubwa kwa timu yao hivyo wameamua kusema ‘Our Teame Our Time’ wakimaanisha timu yao na wakati wao wakuipeperusha bendera ya Tanzania.

Mbali na hayo klabu hiyo imeingia makubaliano ya mashirikiano na serikali yakufanya kampeni za kuondoa magonjwa ya Mlipuko .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here