Home BUSINESS WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefika katika Soko la Kariakoo ambako wafanyabiashara wametangqza mgomo tangu asubuhi na kuzungumza nao.

Waziri Majaliwa amesema kuwa amelazimika kuacha Bunge na kuja kwa dharura ili kuzungumza na wafanyabishara hao kwa lengo la kupata suluhu.

Awali taarifa kutoka katika Ofisi yake ilisema kuwa kiongozi hiyo angekutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko hilo siku ya Jumatano Mei 17, 2023.

Katika mkutano huo Waziri Mkuu Majaliwa alipanga kukutana pia na mawaziri wa sekta hiyo pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye Ofisi yake Magogoni – Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

Hata hivyo, wafanyabiashara hao hawakusitisha mgomo huo na kudai kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan.

Previous articleRAIS SAMIA ATOA NDEGE KUUSAFIRISHA MWILI WA ‘LEMUTUZ’
Next articleSERIKALI YATOA BILIONI 99.3 KUTEKELEZA MIRADI YA KIMAENDELO MKOA WA GEITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here