Home LOCAL WAZAZI WATAKIWA KUENDELEZA NDOTO ZA WATOTO WAO BADALA YA KUWAKATISHA TAMAA

WAZAZI WATAKIWA KUENDELEZA NDOTO ZA WATOTO WAO BADALA YA KUWAKATISHA TAMAA

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Mzumbe ,Rose Joseph akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Mwanafunzi akipata elimu kutoka kwa mmoja wa maafisa katika chuo kikuu cha Mzumbe wakati alipotembelea  banda hilo katika maonesho hayo  jijini  Arusha. 
Julieth Laizer, Fullshangwe Blog -Arusha.
Baadhi ya wazazi nchini wametakiwa kutoa motisha kwa watoto wao na kuendeleza ndoto  zao na kuacha tabia ya kuwachagulia watoto fani ya kusomea kwani kwa kufanya hivyo kunashusha hari na ufanisi  katika kujituma kwenye masomo yao.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko Chuo kikuu Mzumbe  Rose Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari  katika maonesho ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi  yanayoendelea kufanyika jijini Arusha.
Amesema kuwa,watoto wengi wamekuwa na ndoto zao ila wazazi ndio wamekuwa wakiwakwamisha kwa kuwachagulia  fani za kusomea badala ya kuwapa watoto uhuru kusoma kile wanachokipenda wao wenyewe. 
“wapo wazazi ambao hawawapi mtoto nafasi ya kumsikiliza anapenda kusomea fani gani na hivyo mtoto kujikuta akiingia kwenye masomo ambayo hayataki ambapo hali hiyo hudhoofisha kiwango cha  ufaulu na ufanisi wa mtoto”.amesema .
Rose amesema wao kama  chuo cha Mzumbe wanajitahidi kuhakikisha mtoto anapofika Chuoni hapo kwanza wajue anachokipenda ambapo hali hiyo huwalazimu kama chuo kumhamisha mtoto na kumpeleka kwenye bunifu anayoifurahia yeye.
“Tushirikiane kwa pamoja wazazi kutambua matakwa ya mtoto na sio kuwa sehemu ya kutaka mtoto afanye wanachotaka wazazi hiyo imekuwa changamoto kubwa”amesema Rose.
Akizungumzia shughuli wanazofanya Chuo kikuu cha Umma cha Mzumbe ambacho pia wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali  amesema wanawezesha taasisi za elimu ya juu na ufundi stadi ambapo wanatoa elimu kuanzia ngazi ya  cheti .
Amesema kuwa , chuo hicho kimekuwa kikizalisha viongozi na watu mbalimbali kutokana na elimu wanayoitoa na wanajivunia kuwepo kwenye maonyesho hayo ya elimu kwa kuwa hakuna mahali utakapo pita usikutane na zao la Chuo cha Mzumbe.
“Sisi tunaweza kusema tunatembea kifua mbele kwa kuwa tuna watu waliopita hapa Chuoni ikiwemo Rais wa sasa Dkt Samia suluhu Hassan ni zao la Chuo hiki,Spika mstaafu Anna Makinda pia ni zao letu kwa hiyo tunajivunia kwa kweli”amesema Rose.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here