Home LOCAL VIJIJI VITATU GAIRO KUONDOKANA NA SHIDA YA MAJI 

VIJIJI VITATU GAIRO KUONDOKANA NA SHIDA YA MAJI 

NA: FARIDA MANGUBE, GAIRO, MOROGORO 

Wakazi zaidi ya 6,000 kutoka kata tatu za Ibuti, Ngiloli na Tabu hotel Wilaya Halmashauri ya Gairo mkoani Morogoro wanatarajiwa kuondokana na shida ya upatikanaji wa Maji Safi na Salama utakapokamilika mradi mkubwa wa Maji, unaohusisha upanuzi wa miondombinu.

Mradi huo ukianza kutekelezwa tangu mwezi Octoba mwaka 2020, unatekelezwa na Serikali kupitia wakala wa Maji na Usafi wa mazingira vijjijini (RUWASA) kwa fedha za program ya lipa kutokana na matokeo (PbR)  na umepanga kukamilika mwaka huu 2023.
Meneja wa RUWASA Wilaya ya Gairo Mhandisi Isack Gilbert akisoma taarifa wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea mradi  huo, amesema utekelezaji wake umefikia aslimia 85 ukijumuisha ujenzi wa Tangi lenye Lita za ujazo 100, uwekaji wa uzio eneo la Tangi, uwekaji wa mabomba ya kusambaza maji Kilometa 10.1, kuhamisha vituo vya kuchotea maji pamoja na kuunda chombo cha jumuiya ya watumia maji.
“Mradi huu unalenga kupunguza chagamoto ya kutembea umbali mrefu kwa wakazi zaidi ya elfu 6 wa vijiji vya Ngiloli, Ibuti na Tabu Hotel kwenda kutafuta maji safi na salama na kuondoka na magonjwa ya mlipuko.” Amesema Meneja wa RUWASA Wilaya ya Gairo.
Amesema mradi utawasaidia kuongeza kipato kwa wakazi wa maeneo hayo kwani awali walikuwa wanatumia muda mwingi kutafuta maji safi na salama hivyo kukamilka kwa mradi huo kutoka muda kufanya shughuli za kiuchumi na jamii.
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim aliwataka viongozi wanaosimamia miradi ya maendeo kutanguliza uzalendo kwanza na kusimamia miradi inayotekelezwa na kuhakikisha inakuwa kwenye ubora inayokubalika.
Akiwa katika Mradi wa upanuzi wa mioundombinu ya maji vijiji vya Ngiloli, Ibuti na Tabu hotel kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka  2023 Abdulla Shaib Kaim amesema ameridhishwa na utekelezaji wa Mradi pamoja na matumizi ya fedha.
“Niwapongeza Sana ndugu zangu wa RUWASA kwa kazi kubwa na zuri mnayoifanya ya kuhakikisha wananchi waishio vijiji wanapata maji Safi na salama.alisema Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Pia mwenge wa uhuru mwaka 2023 katika wilaya ya Gairo ulitembelea na kuweka jiwe la msingi mradi wa zahanati ya kijiji cha Tabu hotel ambao utekelezaji wake umefikia aslimia 93 na Hadi kukamilika umepangwa kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 71.7 ilukilenga kuboresha huduma za matibabu kwa wakazi zaidi ya elfu 2, 270 waliokuwa wakilazimika kupata huduma umbali wa zaidi ya kilomita 7 kijiji jirani.
Baadhi yao wakazi wa kijiji cha Tabu Hotel kulikojengwa Zahanati hiyo  wameishukuru serikali kwa kutekeleza mradi wakisema kwa MIAKA yote wamekua wakifuata huduma umbali mrefu hasa kwa Amina mama, wajawazito na watoto.
Katika wilaya ya Gairo mwenge wa uhuru mwaka 2023 umetembelea jumla ya Miradi  tisa yenye thamani ya zaidi ya shilingi  Milioni 600.4.
Mwisho.
Previous articleBAJETI YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA 2023/24 TRILIONI 1.2
Next articleKLABU MBALIMBALI ZA SOKA ZAALIKWA KUSHIRIKI MNENE CUP
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here