Home LOCAL UWT KIMANGA WAZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MITI

UWT KIMANGA WAZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MITI

Na: Heri Shaaban (Ilala)

UMOJA wanawake (UWT) Kimanga Jimbo la Segerea wamezindua Kampeni ya kupanda miti kwa kushirikiana na Kamati za Utekelezaji za kata na Matawi .

Kampeni hiyo ya kupanda miti ilizinduliwa na Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala Rukia Mwenge ambapo walipanda miti shule ya Msingi Tumaini na Kimanga .

Mwenyekiti wa Umoja wanawake Kimanga Dkt ,Marysia Tukay, alisema kampeni ya kupanda miti Kimanga ni endelevu kwa ajili ya kutunza Mazingira Kimanga iwe ya kijani .

“Tumezindua Kampeni ya kupanda miti Kimanga ya kijani Umoja wanawake Kata ya Kimanga kwa kushirikiana na Diwani wetu Mlezi Rukia Mwenge na viongozi wa chama katika Juhudi za kuunga mkono Serikali katika utunzaji Mazingira “alisema Tukay

Alipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuwapatia miti kufanikisha kampeni ya utunzaji Mazingira Kata ya Kimanga Wilayani Ilala .

Alitumia nafasi hiyo akiwataka Wanawake wawe chachu ya Maendeleo watumie fursa mbalimbali katika kujikwamua kiuchumi wasiwe tegemezi wawe na miradi yao ya kuwaingizia kipato

Aidha alisema mwaka 2025 Wanawake wote wa Kimanga watampigia kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan

Aliwataka wanawake Mwaka 2024 kujitokeza kwa wingi katika kuchukua fomu kwenye kinyanganyiro cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Wanawake ni Jeshi kubwa ,Wanawake ni nguvu ya chama ,naomba Wanawake wezangu wa Kimanga tushirikiane na Mbunge wetu Bonah Ladslaus Kamoli ,anafanya mambo makubwa kwenye Maendeleo Jimbo letu la Segerea Utekelezaji wa Ilani na miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo sekta ya Elimu ,sekta ya afya na Miundombinu ya Barabara “alisema .

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala ,Rukia Mwenge, aliwataka wanawake na Jamii ya Kimanga kupanda Miti ya matunda na vivuli kila kaya kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji na kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi .

Diwani Rukia Mwenge alisema, mazingira ni muhimu kwa jamii hivyo lazima wakumbushwe wajibu wao wa kupanda miti na kutunza Mazingira .

Aliwaoongeza Umoja wanawake UWT Kimanga kwa kushirikiana pamoja kufanikisha kampeni ya utunzaji mazingira ndani ya Kata hiyo.

Rukia mwenge alisema Kimanga ya kijani inawezekana kampeni hiyo ni endelevu kuibadirisha Kimanga katika kupanda miti mbalimbali .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here