Afisa Rasilimali watu Mwandamizi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Bi. Leah Mwankusye akizungumza na waandishi wa habari katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kimkoa yamefanyika kwenye Uwanja wa Uhuru leo Mei 1,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa Migodi wa STAMICO Mbaraka Haroun akizungumzia ushiriki wao kwenye Maadhimisho hayo alipohojiwa na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Shirika la madini la Taifa (STAMICO) wakiwa kwenye maandamano katika Maadhimisho hayo.
Watumishi wa Shirika la madini la Taifa (STAMICO) wakiwa kwenye picha ya pamoja.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
DAR ES SALAAM.
Katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki maadhimisho hayo kwa kutambulisha Bidhaa yake mpya ya Nishati ya kupikia ya Mkaa mbadala unaotengenezwa na mabaki ya makaa ya mawe (Coal Briquettes)
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Mei 1, 2023 Jijini Dar es Salaam, Afisa Rasilimali watu Mwandamizi wa Shirika hilo Bi. Leah Mwankusye amesema wanatumia Maadhimisho hayo kutambulisha Bidhaa hiyo ikiwa ni sehemu ya kuokoa mazingira katika nchini.
“Niiombe Serikali iendelee kutuunga mkono kama Shirika la Madini ili tuweze kufanya kazi katika ubora zaidi, hivyo basi wananchi watumie mkaa huu kwa ajili ya kuhifadhi mazingira,” amesema.
Ameeleza kuwa Shirika linaendelea na mikakati yake ya kuutangaza mkaa huo na kuhakikisha unazasambaa nchi nzima ili kila mwananchi aupate na kwamba, hatua hiyo itasaidia kuondokana na matumizi ya nishati nyingine zinazoharibu mazingira.
kwa upande wake Mhandisi Migodi wa STAMICO, Mbaraka Haroun amesema kuwa Shirika hilo limejipanga vema katika uzalishaji wa Bidhaa hiyo kutokana na mitambo ya kisasa inayotumika kuondoa simu na kufanya Bidhaa hiyo iwe salama kwa mtumiaji.
“Tuna mtambo wa majaribio ambao upo SIDO unazalisha tani 2 kwa saa, tumeagiza mitambo mingine miwili, mmoja tutafunga Pwani na mwngine tutafunga Mbeya, hii mitambo ni kwaajili ya uzalishaji mkubwa ambao kila mtambo una uwezo wa kuzalisha tano 20 kwa saa, lengo ni kuweka mtambo kila Mkoa ili Wananchi wahifadhi mazingira kwa kutokata miti ovyo na kufanya Tanzania iwe nzuri zaidi,”
“Mkaa huu ni rafiki wa mazingira kwa kuwa unatengenezwa kwa kuchimbwa, na kuupitisha kwenye mtambo ili kutoa sumu. Hviyo ni Mkaa salama, hauna moshi wala harufu” amesema Haroun