NA: TIMA SULTAN
RUVU Shooting imekuwa timu ya kwanza kushuka Daraja na kuiaga rasmi Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.
Mchezo huo wa raundi ya 28 Ligi Kuu umechezwa leo usiku Uwanja wa Azam Complex , Chamazi, Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Mchezo huo yamefungwa na Clatous Chota Chama dakika ya 30 akimaliazia vema krosi ya chini chini ya nahodha, Mohammed Hussein, huku mabao mengine mawili yakiwekwa kimiani dakika ya 72, 90+3 na Pape Sakho ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Jean Baleke.
Katika mtanange huo Jonas Mkude wa Simba alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo mpinzani wake, William Patrick.
Dakika kadhaa kabla ya mchezo huo kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho ‘ alisema wanahitaji ushindi katika nchezo huo ni kurudisha imani ya mashabiki .
“Tunahitaji ushundi kwenye mchezo huu tunajua kwamba hautakuwa mchezo rahisi lakini kwa uwezo wa Mungu tutafanya vizuri na nilisha zungumza na wachezaji wangu juu ya umuhimu wa mchezo huu,” amesema Robertinho
Ruvu Shooting kwenye msimamo wa Ligi hiyo ya NBC wanashika nafasi ya 16 wakiwa na jumla ya Pointi 20Â ambapo kimahesabu tayari .
Hiyo inatoka na uhalisia kwamba hata ikitokea wameshinda mechi mbili za mwisho watafikisha pointi 26, alama moja nyuma ya Mbeya City ambayo ina mechi tatu mbeleni.
Ikumbukwe timu mbili zenye pointi chache zinashuka daraja moja moja kwa moja kwenda kucheza Ligi Daraja la Kwanza.
Kwa upande mwingine timu nyingine ambayo iko kwenye wakati mgumu kama isipo changa vema karata zake kwenye mechi zake tatu itaungana na Ruvu Shooting ni Polisi Tanzania yenye alama 22.