Home BUSINESS SERIKALI YAWATAKA WANANCHI TARIME KUHESHIMU MAENEO YA HIFADHI

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI TARIME KUHESHIMU MAENEO YA HIFADHI

Serikali imewataka wananchi Wilayani Tarime Mkoani Mara kuheshimu maeneo ya Hifadhi kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema hayo Mei 6,2023 katika kijiji cha Gibaso Kata ya Kwihancha wakati wa ziara ya Mawaziri Watatu kutoka Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi ya Serengeti.

Amesema kuwa mwananchi yeyote haruhusiwi kukanyaga hifadhini, kutokana na kuwepo kwa wanyama wakali na changamoto za majangili

“Nimesikia hapa kuna malalamiko mengi pindi mnapoingia ndani ya Hifadhi, Naomba kuwaeleza kuwa eneo lile linatunzwa kwa sheria za nchi na hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kibinadamu” Mhe. Masanja amesisitiza.

Aidha, amefafanua kuwa kazi ya Askari wa Uhifadhi walio katika maeneo ya Hifadhi ni kulinda Hifadhi pamoja na rasilimali zilizomo hifadhini na si vinginevyo.

Amewaasa wananchi hao kuacha tabia ya kuwalaumu Askari Uhifadhi na badala yake waheshimu sheria za nchi kwa kuacha kuingia katika maeneo hayo

Mhe. Masanja amewataka wananchi kukaa katika maeneo ya vijiji yanayoruhusiwa kwa shughuli za kibinadamu.

“Kaeni kwenye maeneo yanayoruhusiwa yaacheni maeneo ya hifadhi yahifadhiwe na wataalamu waliokasimiwa madaraka na Serikali” Mhe. Masanja amesema.

Previous articleRAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA VIONGOZI MBALIMBALI KUANZA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Next articleSERIKALI YAAHIDI KUTOA MIRADI YA UJIRANI MWEMA KWA VIJIJI VITAKAVYOONGOZA KUDHIBITI UJANGILI WA WANYAMAPORI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here