Home BUSINESS SAUT WAHAMASISHWA KUHUSU MILIKI UBUNIFU

SAUT WAHAMASISHWA KUHUSU MILIKI UBUNIFU

.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT) cha Jijini Mwanza, Prof. Costa Mahalu (kulia) akizungumza na Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA) walipomtembelea ofisini kwake kabla ya mafunzo ya Miliki Ubunifu kwa Wahadhiri na Wanafunzi wa chuo hicho tarehe 9 Mei, 2023. ameipongeza BRELA kwa kuandaa mafunzo hayo na kufika katika Chuo hicho ambacho kinafundisha taaluma mbalimbali ikiwemo Miliki Ubunifu na Elimu ya Biashara.
 Prof. Mahalu ameipongeza BRELA kwa kuandaa mafunzo hayo na kufika katika Chuo hicho ambacho  kinafundisha taaluma  mbalimbali ikiwemo Miliki  Ubunifu na Elimu ya Biashara.

Msaidizi wa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Nasoro Mtavu akizungumza na Wahadhiri pamoja na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) tarehe 09 Mei, 2023 katika ukumbi wa Chuo hicho Jijini Mwanza, kuhusu sajili  zote za Miliki Ubunifu  zinazosimamiwa na kulindwa na BRELA ambazo hufanyika kupitia mfumo wa Usajili kwa  njia ya Mtandao ( Online Registration System-ORS),  unaopatikana katika tovuti ya BRELA, www.brela.go.tz lengo likiwa ni kuokoa muda na kupunguza gharama.

Wanafunzi na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) wamehamasishwa kuchagua maeneo ya kubobea katika taaluma ya Kisayansi ili waweze kuandika maandiko mbalimbali ya maombi ya hataza.
MWANZA

Hamasa hizo zimetolewa na Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Stanslaus Kigosi wakati akitoa elimu ya Miliki Ubunifu chuoni hapo tarehe 9 Mei, 2023 jijini Mwanza.

Bw. Kigosi amesema kwa sasa kuna uhaba wa wataalam wa kuandaa maandiko ya maombi ya Hataza, hivyo wakibobea katika maeneo hayo watanufaika.

Bw. Kigosi ameshauri pia ni vyema Wanafunzi wa Kada mbalimbali wakaona umuhimu wa kushiriki mafunzo kama haya kwasababu maisha ya binadamu kila siku yanazungukwa na kazi za Miliki Ubunifu ambazo kimsingi ni chanzo cha mapato kwa wabunifu na watumiaji wa kazi za Miliki Ubunifu.

“Mtu akiwa na uelewa wa Miliki Ubunifu atajua namna bora ya kulinda ubunifu wake na namna bora ya kuingiza ubunifu wake kwenye soko la ndani na nje”, amefafanua Bw. Kigosi.

Naye Afisa Mwandamizi kutoka BRELA Bw. Raphael Mtalima amesema kuwa SAUT inafanya tafiti mbalimbali ambazo matokeo yake yanaweza kufanyiwa mchakato wa kuwa bidhaa au namna za kutengeneza vitu mbalimbali hivyo, wakilinda vumbuzi hizo zitakuwa na manufaa kwa mbunifu, chuo na jamii kwa ujumla.

Ameongeza kwa mifano kuwa haki za Miliki Ubunifu ikiwemo Hataza na Alama za Biashara na Huduma zimekuwa na thamani ulimwenguni hivyo Bunifu wanazo zianzisha au zibuni wazisajili BRELA ili zilindwe na ziweze kunufaisha na kusaidia jamii.

Aidha ,Msaidizi wa Usajili wa BRELA Bw. Nasoro Mtavu amesema kuwa Usajili wa Miliki Ubunifu zote zinazosimamiwa na kulindwa na BRELA zinafanyika kwa njia ya mtandao ambao unapatikana katika tovuti ya www.brela.go.tz lengo ikiwa ni kuokoa muda na kupunguza gharama.

Awali akitoa neno la ukaribisho Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Costa Mahalu amewapongeza BRELA kwa kuandaa mafunzo hayo ya Miliki Ubunifu na kufika katika Chuo hicho ambacho kinafundisha taaluma mbalimbali ikiwemo ya Miliki Ubunifu na Elimu ya Biashara

Pia amewataka BRELA kuendelea kufika katika chuo hicho pale wanapopewa mialiko na kutoa mafunzo kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA.

Kwa upande wake Dkt. Samwel Mseti , ambaye ni Mhadhiri wa Masomo ya Biashara, SAUT amewashukuru BRELA kwa mafunzo ya Miliki Ubunifu kwa wanafunzi na watumishi kwani Chuo Kikuu ni taasisi ya kutoa elimu kwa nadharia na vitendo, hivyo ujio wa BRELA unakamilisha dhana ya kutoa elimu kwa vitendo.

Previous articlePATA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 10, 2023
Next articleJE UNAFAHAMU MAANA NA UMUHIMU WA RANGI NYEKUNDU KATIKA TIMU ZA SOKA?
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here