Home LOCAL RUWASA WAPONGEZWA MUSOMA VIJIJINI

RUWASA WAPONGEZWA MUSOMA VIJIJINI

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), unapatanua huduma zake kutoka Bomba la linalopeleka Maji Bujaga – Bulinga – Busungu katika Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara kwenda Kata ya Bwasi, Vijiji vya Bugunda, Kome na Bwasi.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo, Mradi huo unaogharimu Sh 997,714,196 una urefu wa mtandao wa usambazaji maji wa Kilomita 31.5 na Vitekea maji 35.

“Linajengwa Tenki lenye ujazo wa Lita 150,000 kwenye Kijiji cha Bwasi na tunatarajia kabla ya Juni 30 Mwaka huu, mradi uwe umekamilika,” amesema Prof Muhongo.

Amesema vijiji vyote 68 vya Jimbo hilo vina miradi ya maji ambayo iko kwenye hatua tofauti za utekelezaji na kwamba maji yanayosambazwa katika Bomba hilo la Bujaga – Bulinga – Busungu, yanatolewa Ziwa Victoria.

Amesema licha ya mashine ya kusukuma maji hayo kujengwa kijijini Bujaga, Kata ya Bulinga kuna Tenki lenye ujazo wa Lita 200,000 limejengwa kijijini Busungu na lingine lenye ujazo wa Lita 150,000 limejengwa kijijini Bulinga ndani ya Kata hiyo.

Amesema matenki hayo pia yanasambaza Maji kwenye vijiji vya Bukima, Kata ya Bukima na Kwikerege Kata ya Rusoli na kwamba kwa niamba ya wakazi wa Jimbo hilo, anashukuru kwa dhati Serikali ya awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kusambaza Maji Safi na Salama mabombani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here