Home SPORTS RAIS SAMIA KUTOA MILIONI 20 KWA KILA GOLI LA YANGA SC FAINALI...

RAIS SAMIA KUTOA MILIONI 20 KWA KILA GOLI LA YANGA SC FAINALI YA CAF

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutoa zawadi ya Shilingi Milioni 20 kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Yanga SC katika mchezo wao wa fainali za Mashindano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation)

Rais Samia ametoa ahadi hiyo leo Mei 18, 2023 katika hafla ya uzinduzi wa mradi ujenzi wa minara 21 ya Kampuni ya AZAM (DTT) iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Awali nilikuwa nikitoka Milioni 5 kwa kila goli, na baadae nikaongeza ikawa 10, sasa kila goli ni Shilingi Milioni 20 kwa matokeo ya ushindi” amesema RAIS Samia.

Aidha ameahidi kutoa ndege itakayowasafirisha wacheza, viongozi pamoja na mashabiki kwenda kwenye mchezo wa fainali na kuwarudisha.

Yanga SC itacheza dhidi ya USM Algers ya Algeria hatua ya fainali, ambapo mkondo wa kwanza utapigwa Mei 28 Jijini Dar es Salaam na kurudiana Juni 03, 2023 nchini Algeria. 

Previous articleCWT SERENGETI KITENGO CHA WANAWAKE CHA WEZESHA UPATIKANAJI WA MAJIKO 190 YA GESI
Next articleWAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA BENKI YA CRDB KWA KUTOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI KUIMARISHA USALAMA KWA WATALII JIJINI ARUSHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here