RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutoa zawadi ya Shilingi Milioni 20 kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Yanga SC katika mchezo wao wa fainali za Mashindano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation)
Rais Samia ametoa ahadi hiyo leo Mei 18, 2023 katika hafla ya uzinduzi wa mradi ujenzi wa minara 21 ya Kampuni ya AZAM (DTT) iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
“Awali nilikuwa nikitoka Milioni 5 kwa kila goli, na baadae nikaongeza ikawa 10, sasa kila goli ni Shilingi Milioni 20 kwa matokeo ya ushindi” amesema RAIS Samia.
Aidha ameahidi kutoa ndege itakayowasafirisha wacheza, viongozi pamoja na mashabiki kwenda kwenye mchezo wa fainali na kuwarudisha.
Yanga SC itacheza dhidi ya USM Algers ya Algeria hatua ya fainali, ambapo mkondo wa kwanza utapigwa Mei 28 Jijini Dar es Salaam na kurudiana Juni 03, 2023 nchini Algeria.