Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Mradi wa Minara ya kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Ltd, Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo wakati Mtoto Georgina Magesa (8) akiwa ameketi kwenye Kiti cha Rais mara baada ya kukutana naye katika hafla ya uzinduzi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Azam Media iliyofanyika katika Ofisi zao zilizopo katika Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Bi Hadija Said Mtangazaji wa kwanza Mwanamke nchini akihudumu katika Redio ya Taifa (RTD) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Mama Violet Maro Mwanamke wa kwanza Mwandamizi katika fani ya Habari nchini wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Mama Debora Mwenda Mtangazaji wa kwanza Mwanamke kuandaa vipindi vya Watoto wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Mama Eda William Sanga, Mtangazaji wa kwanza Mwanamke kutangaza Taarifa ya habari ya Tanzania kupitia Redio Tanzania (RTD) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) Tabata Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.