Home LOCAL RAIS DKT. SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA MEI MOSI MOROGORO

RAIS DKT. SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA MEI MOSI MOROGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono viongozi pamoja na Wafanyakazi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa zimefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.
Wafanyakazi kutoka Wizara, Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.
Wafanyakazi kutoka Wizara, Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi wakiwa kwenye Maandamano wakati wakiingia kwenye uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya pamoja na Viongozi wengine wakiimba Wimbo wa Mshikamano (Solidarity) wakati wa Sherehe ya Mei Mosi ambazo Kitaifa zimefanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro tarehe 01 Mei, 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here