Home Uncategorized ORYX GAS KUENDELEA KUIUNGA TULIA TRUST MASHINDANO YA MBIO ILI KUPATA FEDHA...

ORYX GAS KUENDELEA KUIUNGA TULIA TRUST MASHINDANO YA MBIO ILI KUPATA FEDHA KUSAIDIA WATOTO WA KIKE MBEYA

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit akishiriki mbio za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit kulia akivishwa medali baada ya kukimbia mbiop za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu Mkoani Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ambayo ni msimu wa saba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit wa pili kushioto akiwa  na baadhi ya wabunge baada kushiriki kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oryx Gas Tanzania Arama Benoit akiwa na baadhi wa watumishi wa kampuni hiyo walioshiriki mbio za kilomita tano katika mashindano ya Tulia Marathoni yaliyofanyika jijini Mbeya kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya na elimu yaliyofanyika jijini Mbeya na kampuni ya Oryx Gas wakiwa wadhamini wenzi katika mashinadno hayo ukiwa ni msimu wa saba.

Na: Mwandishi Wetu, MBEYA

KAMPUNI ya Oryx Gas imesema itaendelea kuiunga mkono Taasisi ya Tulia Trust katika mashindano ya riadha inayoyaratibu kwa kuwa malengo yake yanafanana na ya kampuni hiyo katika kuisaidia jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Benoite ameeleza hayo leo Mei 6,2023 baada ya kuwaongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kushiriki mashindano ya riadha yaliyoratibiwa na Taasisi ya tulia Trust na yaliyofanyika jijini Mbeya.

Amesema kuwa Oryx Gas kwa kipindi kirefu imejikita katika huduma za jamii hususani zinazohusu kuisaidia jamii ya Watanzania na zaidi mtoto wa kike kwa kuhakikisha anaondokana na changamoto mbalimbali ,hivyo wameona iko haja kuungana na Tulia Trust katika kumsaidia mtoto wa kike katika afya na elimu ndani ya Mkoa huo.

Akieleza zaidi kuhusu ushiriki wao katika mbizo hizo Araman amefafanua kuwa Kampuni ya Oryx Gas imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kumuondolea changamoto mwanamke ,hivyo kwenye mashindano ya mbio hizo ni wazi malengo ya taasisi hiyo yanafanana na yao,hivyo wataendelea kuunga mkono.

Amefafanua katika kutekeleza hilo kwa vitendo Kampuni ya Oryx imekuwa na kampeni ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia kwa kugawa majiko na mitungi ya gesi kwa wanawake wa mikoa mbalimbali ambapo hadi sasa wamewafikia zaidi ya 5,000, lengo ni kuhakikisha wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa.

“Hivyo tunapoona Taasisi ya Tulia Trust inandaa mbio za kuchangisha fedha kuisaidia jamii ya mtoto wa kike, sisi tunaona ni wajibu wetu kusaidia kwa kufadhili ili mambo yaende kama yalivyopangwa na fedha zinazopatikana zinakwenda kugusa maisha ya wenye uhitaji, tutaendelea kushirikiana na taasisi hii itimize malengo yake,”amesema.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Oryx Gas wakiongozwa na Benoite wameshiriki mbizo hizo huku mkurugenzi mtendaji huyo akieleza jinsi Kampuni hiyo inavyofurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Tulia Trust katika kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya Watanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here