Home LOCAL MWILI WA MKONO WAWASILI

MWILI WA MKONO WAWASILI

Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Sagini leo 27 Mei, 2023  ameongozana na Wanafamilia, Ndugu, Jamaa na  Marafiki wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama Mkoani Mara  Nimrod  Mkono ambaye mwili wake umewasili leo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere  kutokea Nchini Marekani ambapo alikuwa akipatiwa matibabu tangu mwaka 2018 na kufariki 18 Aprili, 2023. 
Mara baada ya kupokelewa kwa mwili huo mapema leo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwili huo  ulipelekwa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ibada na kesho tarehe 28 Mei, 2023 mwili wa marehemu Wilbroad mkono utaagwa katika Viwanja vya Karimjee na hatimaye kusafirishwa kwenda Kijijini kwao Busegwe Wilaya ya Butiama Mkoani Mara kwa ajili ya shughuli za mazishi siku ya Jumatatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here