Home BUSINESS MSTAHIKI MEYA ASISITIZA VIJANA WA TEMEKE KUSAIDIWA KIBIASHARA

MSTAHIKI MEYA ASISITIZA VIJANA WA TEMEKE KUSAIDIWA KIBIASHARA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imesisitizwa kusaidia vijana wa Wilaya ya Temeke ili waweze kurasimisha biashara zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Abdallah S. Mtinika, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke alipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Kijana Janjaruka Festival Temeke ya Fursa leo tarehe 21 Mei, 2023 katika uwanja wa Zakhiem Mbagala.

Mhe. Mtinika ameiomba BRELA isaidie vijana katika kutoa mafunzo mbalimbali ili waweze kutumia fursa zilizopo wilaya ya Temeke

“BRELA muandae programu mbalimbali za kuwashirikisha vijana wa Temeke ili waweze kutoka kwenye utegemezi na kufikia hatua ya kujisimamia kwa kuwa fursa zipo nyingi” amesisitiza Mhe. Mtinika

Naye Nassoro Mtavu, Msaidizi wa Usajili Mwandamizi kutoka BRELA, ameeleza kuwa BRELA inatoa mafunzo kuanzia ngazi za vyuoni na pia wale walio nje ya mfumo wa elimu, huwafikia kwa kushiriki kwenye matukio mbalimbali yanayoratibiwa kuanzia ngazi za wilaya.

“Kwa upande wa vyuoni vijana wamekuwa na bunifu zao bila ya kujua namna ambavyo wanaweza kuzilinda bunifu hizo na kuzitumia kibiashara” amesema Bw. Mtavu

Bw. Mtavu amesisitiza kuwa BRELA imeweza kutambua mchango wa vijana hao hasa kupitia maadhimisho ya siku ya Miliki Ubunifu Duniani ambapo Tanzania iliadhimisha tarehe 28 Aprili,2023 kupitia alama zao walizosajili, BRELA ilitambua ubunifu wao na kuwatunukia tuzo ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika ukuaji wa sekta ya biashara nchini, kutoa ajira na kuwepo kwa alama ya biashara ambayo bidhaa yake imedumu kwenye soko la biashara kwa muda mrefu

BRELA inashiriki kwenye Maonesho ya Kijana Janjaruka Festival Temeke ya Fursa kwa kutoa huduma mbalimbali za Sajili, utoaji wa Leseni na huduma baada ya Sajili. Maonesho haya yanatarajiwa kufungwa tarehe 24 Mei,

Previous articleBARRICK YADHAMINI KONGAMANO LA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA IRINGA
Next articleCCM YATOA TAARIFA YA KIKAO CHA KAMATI KUU,YAMPONGEZA MWENYEKITI WAKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here